Katika kipindi ambacho dunia inakabiliwa na changamoto za upatikanaji wa mafuta na kupanda kwa gharama za nishati, matumizi ya magari yenye teknolojia inayowezesha kupunguza utegemezi wa mafuta yanaendelea kuwa sehemu muhimu ya kukabiliana na changamoto hiyo.
Tanzania nayo haiko nje ya mazingira hayo, huku Serikali chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ikiendelea kuhimiza matumizi yenye ufanisi ya nishati na kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ya mafuta.
Katika kuunga mkono jitihada hizo za Serikali na kuwapa Watanzania fursa ya kutumia usafiri unaozingatia matumizi bora ya nishati, JETOUR Tanzania imezindua JETOUR Club pamoja na kutambulisha magari mawili mapya yenye teknolojia ya plug-in hybrid, JETOUR G700 na JETOUR F700, yanayochanganya matumizi ya umeme na mafuta.
Hatua hiyo inalenga kuongeza chaguo kwa Watanzania wanaohitaji magari yenye uwezo wa kusafiri katika mazingira mbalimbali huku yakitoa fursa ya kutumia umeme katika safari fupi na mafuta katika safari ndefu, tofauti na magari yanayotegemea mafuta pekee.
Uzinduzi huo umefanyika chini ya kaulimbiu ya “Africa Expedition 2025”, ukiwa sehemu ya mpango wa JETOUR Tanzania, kwa kushirikiana na Africarriers Group, wa kuimarisha uwepo wa chapa hiyo katika soko la Tanzania na wakati huo huo kuunganisha teknolojia ya magari ya kizazi kipya na uzoefu mpana wa umiliki.

No comments:
Post a Comment