Wanawake, Vijana, Wazee na Watu wenye mahitaji maalum wa mikoa ya Kanda ya Kusini wametakiwa kuchangamkia fursa zinazopatikana katika zabuni za Umma ili kuongeza ushiriki wao katika shughuli za kiuchumi na maendeleo ya taifa.
Wito huo umetolewa na Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Lindi, Bi. Alusaria Mushi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Adam Malima katika Kongamano la Viwanda, Uwekezaji, Teknolojia na Uvumbuzi kwa Wanawake, Vijana, Wazee na Watu wenye mahitaji maalum wa mikoa ya Kanda ya Kusini lililoratibiwa na Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) jana mkoani Lindi.
Bi. Mushi amesema kuwa Serikali imeendelea kuweka mazingira bora ya kuwainua wananchi kiuchumi kupitia mifumo ya ununuzi wa umma ambapo mifumo hiyo imekuwa ikiwawezesha wazabuni kushiriki kwa haki na uwazi, na haki zao zimekuwa zikilindwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za ununuzi wa umma.
“Sheria na Kanuni zinaruhusu mtu au kikundi cha watu wenye mahitaji maalumu kupata fursa ya mkopo wa kategoria ya makundi maalumu ambapo mmetengewa asilimia 30 kwa vijana, wanawake wazee na watu wenye mahitaji maalumu, sasa kazi kwenu wana-Lindi kuchangamkia fursa hiyo. Ila changamoto kubwa ya ninayoiona kwenu kama makundi Maalumu siyo fursa, bali ni utayari wa kuchangamkia fursa hizo,” amesema Bi. Mushi
Aidha, Bi. Mushi ameitaka Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) kuendelea kuwajengea uwezo Vijana, Wanawake, Wazee na Watu wenye mahitaji maalumu uelewa juu ya haki zao katika michakato ya ununuzi wa umma pamoja na matumizi ya mifumo ya kidijitali katika kushughulikia malalamiko na rufaa.
“Naomba PPAA muendelee kuwajengea uwezo vijana, wanawake na watu wenye mahitaji maalumu ili kuwawezesha kujua namna ya kudai haki zao pale wanapoona hawakutendewa haki katika zabuni walizoomba Serikalini, kwani baadhi yao wamekuwa waoga au hawajui mahali pa kudai haki zao,” ameongeza Bi. Mushi
Pamoja na mambo mengine, Bi. Mushi amewasihi washiriki wa kongamano hilo kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotokana na ununuzi wa umma ili kuwawezesha kunufaika kiuchumi na kwa maendeleo yao binafsi na ya Taifa kwa ujumla lakini zaidi kwa maendeleo ya Mkoa wa Lindi.
Kwa upande wake, Mkuu wa Sehemu ya Mashauri kutoka PPAA, Bi. Violet Limilabo ambaye alimwakilisha Katibu Mtendaji wa PPAA, Bw. James Sando katika kongamano hilo, amesema PPAA imeendelea kutoa elimu kwa wadau kuhusu haki na wajibu wa wazabuni katika michakato ya ununuzi wa umma, hususan matumizi ya mifumo ya kidijitali katika kushughulikia malalamiko na rufaa pale wanapoona hawakutendewa haki.
Bi. Limilabo ameongeza kuwa, elimu hiyo inalenga kuongeza uwazi, uwajibikaji na imani ya wadau katika mfumo wa ununuzi wa umma, huku ikichochea ushiriki wa makundi mbalimbali katika shughuli za kiuchumi.
“Kwa sasa PPAA inapokea na kushughulikia malalamiko na rufaa kupitia Moduli ya usimamizi wa Malalamiko na rufaa katika mfumo wa NeST, matumizi ya Moduli hiyo yameleta manufaa mbalimbali ikiwemo kuokoa muda, kupunguza gharama, kuongeza uwazi na uwajibikaji pamoja na kuweka kumbukumbu sahihi za malalamiko na rufaa zinazowasilishwa na wazabuni,” amesema Bi. Limilabo.
Kongamano hilo limewakutanisha takribani wanawake, vijana, wazee na watu wenye mahitaji maalumu 150 na kutoa fursa ya kujifunza, kubadilishana uzoefu na kujenga mitandao ya kibiashara itakayowawezesha kutumia fursa za uwekezaji, teknolojia na ubunifu zinazotanganzwa na Serikali hususani zile fursa zinazopatikana katika Mkoa wa Lindi.
Bi. Limilabo pia ameyahimiza makundi hayo maalumu kuhakikisha yanajisajili katika mfumo wa ununuzi wa umma ili kupata fursa ya kushiriki katika zabuni zinazotangazwa na Serikali.
Aidha, amewataka kuwa tayari kuchukua hatua stahiki pale wanapoona hawajatendewa haki katika mchakato wa zabuni, kwa kuwasilisha malalamiko na rufaa kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa. Hatua hiyo itasaidia Serikali kupata thamani halisi ya fedha katika utekelezaji wa miradi yake na kuhakikisha wananchi wananufaika na miradi hiyo kwa wakati uliopangwa.
.jpeg)
Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Lindi, Bi. Alusaria Mushi akifungua Kongamano la Viwanda, Uwekezaji, Teknolojia na Uvumbuzi kwa Wanawake, Vijana, Wazee na Watu wenye mahitaji maalum wa mikoa ya Kanda ya Kusini lililoratibiwa na Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Adam Malima jana mkoani Lindi.
Mkuu wa Sehemu ya Mashauri kutoka PPAA, Bi. Violet Limilabo akitoa mada kuhusu utatuzi wa migogoro, haki na usawa kwa wote katika michakato ya zabuni za umma katika kongamano la Viwanda, Uwekezaji, Teknolojia na Uvumbuzi kwa Wanawake, Vijana, Wazee na Watu wenye mahitaji maalum wa mikoa ya Kanda ya Kusini lililoratibiwa na Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) jana mkoani Lindi..jpeg)

Sehemu ya washiriki wakifutilia mada kuhusu utatuzi wa migogoro, haki na usawa kwa wote katika michakato ya zabuni za umma katika kongamano la Viwanda, Uwekezaji, Teknolojia na Uvumbuzi kwa Wanawake, Vijana, Wazee na Watu wenye mahitaji maalum wa mikoa ya Kanda ya Kusini lililoratibiwa na Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) mkoani Lindi.jpeg)
Meza kuu katika picha ya pamoja na washiriki wa kongamano la Viwanda, Uwekezaji, Teknolojia na Uvumbuzi kwa Wanawake, Vijana, Wazee na Watu wenye mahitaji maalum wa mikoa ya Kanda ya Kusini lililoratibiwa na Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) mkoani Lindi.
Kwa upande wake, Mkuu wa Sehemu ya Mashauri kutoka PPAA, Bi. Violet Limilabo ambaye alimwakilisha Katibu Mtendaji wa PPAA, Bw. James Sando katika kongamano hilo, amesema PPAA imeendelea kutoa elimu kwa wadau kuhusu haki na wajibu wa wazabuni katika michakato ya ununuzi wa umma, hususan matumizi ya mifumo ya kidijitali katika kushughulikia malalamiko na rufaa pale wanapoona hawakutendewa haki.
Bi. Limilabo ameongeza kuwa, elimu hiyo inalenga kuongeza uwazi, uwajibikaji na imani ya wadau katika mfumo wa ununuzi wa umma, huku ikichochea ushiriki wa makundi mbalimbali katika shughuli za kiuchumi.
“Kwa sasa PPAA inapokea na kushughulikia malalamiko na rufaa kupitia Moduli ya usimamizi wa Malalamiko na rufaa katika mfumo wa NeST, matumizi ya Moduli hiyo yameleta manufaa mbalimbali ikiwemo kuokoa muda, kupunguza gharama, kuongeza uwazi na uwajibikaji pamoja na kuweka kumbukumbu sahihi za malalamiko na rufaa zinazowasilishwa na wazabuni,” amesema Bi. Limilabo.
Kongamano hilo limewakutanisha takribani wanawake, vijana, wazee na watu wenye mahitaji maalumu 150 na kutoa fursa ya kujifunza, kubadilishana uzoefu na kujenga mitandao ya kibiashara itakayowawezesha kutumia fursa za uwekezaji, teknolojia na ubunifu zinazotanganzwa na Serikali hususani zile fursa zinazopatikana katika Mkoa wa Lindi.
Bi. Limilabo pia ameyahimiza makundi hayo maalumu kuhakikisha yanajisajili katika mfumo wa ununuzi wa umma ili kupata fursa ya kushiriki katika zabuni zinazotangazwa na Serikali.
Aidha, amewataka kuwa tayari kuchukua hatua stahiki pale wanapoona hawajatendewa haki katika mchakato wa zabuni, kwa kuwasilisha malalamiko na rufaa kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa. Hatua hiyo itasaidia Serikali kupata thamani halisi ya fedha katika utekelezaji wa miradi yake na kuhakikisha wananchi wananufaika na miradi hiyo kwa wakati uliopangwa.
.jpeg)
Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Lindi, Bi. Alusaria Mushi akifungua Kongamano la Viwanda, Uwekezaji, Teknolojia na Uvumbuzi kwa Wanawake, Vijana, Wazee na Watu wenye mahitaji maalum wa mikoa ya Kanda ya Kusini lililoratibiwa na Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Adam Malima jana mkoani Lindi.

Mkuu wa Sehemu ya Mashauri kutoka PPAA, Bi. Violet Limilabo akitoa mada kuhusu utatuzi wa migogoro, haki na usawa kwa wote katika michakato ya zabuni za umma katika kongamano la Viwanda, Uwekezaji, Teknolojia na Uvumbuzi kwa Wanawake, Vijana, Wazee na Watu wenye mahitaji maalum wa mikoa ya Kanda ya Kusini lililoratibiwa na Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) jana mkoani Lindi.
.jpeg)

Sehemu ya washiriki wakifutilia mada kuhusu utatuzi wa migogoro, haki na usawa kwa wote katika michakato ya zabuni za umma katika kongamano la Viwanda, Uwekezaji, Teknolojia na Uvumbuzi kwa Wanawake, Vijana, Wazee na Watu wenye mahitaji maalum wa mikoa ya Kanda ya Kusini lililoratibiwa na Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) mkoani Lindi
.jpeg)
Meza kuu katika picha ya pamoja na washiriki wa kongamano la Viwanda, Uwekezaji, Teknolojia na Uvumbuzi kwa Wanawake, Vijana, Wazee na Watu wenye mahitaji maalum wa mikoa ya Kanda ya Kusini lililoratibiwa na Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) mkoani Lindi.

No comments:
Post a Comment