HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 16, 2026

Atletico Madrid Dhidi ya Osasuna, Nani kubeba pointi Tatu?

 


WABISHI wa soka LaLiga, Atletico Madrid ya chini ya kocha Diego Simeone, watakuwa wenyeji wa Osasuna usiku huu wa Jumatano, Septemba 16, katika mchezo wa raundi ya sita ya LaLiga utakaochezwa kwenye Uwanja wa Riyadh Air Metropolitano. kuanzia saa 20:00 usiku.

Atlético Madrid inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na kumbukumbu nzuri dhidi ya Osasuna. Katika mikutano ya hivi karibuni, Atletico madrid wameonyesha ubora mkubwa, wakiwa wameshinda mechi nyingi kati yao.

Hata hivyo, kocha Diego Simeone anakabiliana na changamoto za upungufu wa wachezaji, kama Alexander Sørloth ambaye bado hajarejea kutokana na jeraha la misuli. Pablo Barrios pia hayupo baada ya kupata jeraha kwenye mchezo wa Champions League dhidi ya Liverpool.

Osasuna, upande wa pili, inaingia kwenye mchezo huu ikiwa imepoteza mechi yao ya hivi karibuni dhidi ya Espanyol kwa mabao 2-0. Kocha Luis Miguel Ramis atahitaji kuimarisha safu yake ya ushambuliaji ili kuweza kupata matokeo mazuri ugenini. Ante Budimir, ambaye amekuwa akifunga mabao muhimu, atakuwa mchezaji wa kuangaliwa sana katika mchezo huu.

Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema. Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Kwa upande wa msimamo, mechi hii ni muhimu kwa timu zote mbili kutaka kujipenyeza kwenye nafasi za juu za ligi. Atlético Madrid ina pointi 10 baada ya mechi tano, wakati Osasuna ina pointi saba. Ushindi katika mchezo huu unaweza kuipa Atlético nafasi nzuri ya kushiriki katika mbio za ubingwa mbele ya Real madrid na Barcelona.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad