HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, August 20, 2026

NMB YAINGIA AMAMU MPYA YA UBORA WA HUDUMA KWA WATEJA.

Benki ya NMB imekamilisha uhamishaji wa shughuli zake kwenda katika Mfumo Mkuu mpya wa Benki, hatua inayolenga kuongeza uwezo wa kushughulikia miamala, kuimarisha usalama wa taarifa na kuwezesha utoaji wa huduma mpya kwa wateja zaidi ya milioni 10.

Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna, amesema mfumo huo umeandaliwa kwa zaidi ya miaka miwili kupitia majaribio, uhakiki wa teknolojia na tathmini za vihatarishi. Hatua ya mwisho ya kuhamisha taarifa za wateja ilianza Julai 31, 2026.

Mfumo huo unaunganisha akaunti, miamala, mikopo, matawi, mawakala, ATM, NMB Mkononi na huduma nyingine za benki. Zaipuna amewahakikishia wateja kuwa fedha, taarifa na kumbukumbu zao ziko salama, huku uendeshaji wa huduma ukiendelea kuimarika.

Uwekezaji huo unaweka msingi wa utekelezaji wa Mpango Mkakati wa NMB wa mwaka 2026–2030. Kwa sasa, benki hiyo ina matawi zaidi ya 250, mawakala zaidi ya 80,000, ATM zaidi ya 700 na zaidi ya misimbo 130,000 ya QR ya kupokea malipo.





No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad