Na Mwandishi Wetu, Tanga
BARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) limeeleza kuwa mashindano ya ujuzi yanayoendelea nchini ni sehemu ya maandalizi ya kuwaibua vijana wenye uwezo wa kushindana katika viwango vya Afrika na kimataifa kupitia WorldSkills.
Akizungumza Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu jijini Tanga, Katibu Mtendaji wa NACTVET, Dkt. Mwajuma Lingwanda, amesema baraza hilo limeandaa mashindano hayo kuanzia ngazi ya Kanda hadi Taifa, huku hatua ya kitaifa ikiendelea katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara, Tanga.
Amesema jumla ya washiriki 46 kutoka taasisi mbalimbali wamefika katika hatua ya kitaifa, baada ya kufanya vizuri katika hatua za awali za mashindano hayo.
Dkt. Lingwanda, amesema mashindano hayo yamehusisha maeneo tisa ya ujuzi, huku washiriki na majaji wakiwa tayari kwa ajili ya kuendelea na hatua ya kitaifa.
Amesema mashindano hayo yana umuhimu mkubwa katika kuwabaini vijana wenye vipaji na umahiri wa hali ya juu, ambao baadaye watapata fursa ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya ujuzi ya ngazi za juu.
Ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kushuhudia mashindano hayo na kutambua umuhimu wa ujuzi katika kujenga nguvu kazi yenye uwezo na ushindani ndani na nje ya nchi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uthibiti Ubora NACTVET, Dkt. Jofrey Oleke, amesema mashindano hayo yanahusisha fani mbalimbali zikiwemo Upishi, Mekatroniki, Mtandao wa Vitu (IoT), Ujenzi, Uchomeleaji na Uungaji Vyuma, Uhandisi, Urembo na Tiba, Ubunifu pamoja na Teknolojia.
Amesema awali fani 15 zilitangazwa kwa ajili ya kushiriki katika mashindano hayo, lakini baada ya mchakato wa ushiriki na ushindani, fani tisa ndizo zilizofikia hatua ya kitaifa.
Tanzania yajiandaa kwa ushindani wa kimataifa
WorldSkills ni mtandao wa kimataifa unaolenga kukuza ubora wa ujuzi kupitia mashindano, viwango vya mafunzo na ushirikiano kati ya Serikali, waajiri na taasisi za elimu ya ufundi.
Tanzania ilipokelewa rasmi kuwa mwanachama wa WorldSkills Africa mwaka 2025, ikiwakilishwa na NACTVET, hatua ambayo imefungua fursa kwa vijana wa Tanzania kujipima na kushindana kwa kuzingatia viwango vya kimataifa.
Dkt. Lingwanda ametoa shukrani kwa wadau na wafadhili wanaoendelea kuiunga mkono NACTVET katika maandalizi ya mashindano hayo, huku akizitaka kampuni na taasisi mbalimbali kuongeza ushiriki wao kwa kufadhili programu za ujuzi.
Amesema ushirikiano kati ya Serikali, sekta binafsi na wadau wengine ni muhimu katika kuhakikisha vijana wanapata mazingira bora ya kukuza vipaji na ujuzi wao.
Kwa mujibu wa NACTVET, washindi wa mashindano ya kitaifa watapata fursa ya kuiwakilisha Tanzania katika hatua za juu za mashindano ya ujuzi, hivyo mashindano hayo kuwa daraja muhimu la kuwaandaa
Monday, August 17, 2026
Home
HABARI
HABARI JAMII
NACTVET yafungua njia kwa vijana kushindana kimataifa kupitia WorldSkills Tanzania
NACTVET yafungua njia kwa vijana kushindana kimataifa kupitia WorldSkills Tanzania
Tags
# HABARI
# HABARI JAMII
HABARI JAMII
Labels:
HABARI,
HABARI JAMII
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment