AFYA bora ni mtaji wa maisha, lakini kwa baadhi ya makundi katika jamii, kupata mahitaji muhimu ya kila siku bado ni changamoto kubwa. Kwa kutambua hilo, Meridianbet imeendelea kuonyesha kuwa mchezo hauishii uwanjani pekee, bali pia una nafasi kubwa ya kugusa maisha ya watu nje ya uwanja. Safari hii, kampuni hiyo imepeleka nguvu zake za kijamii hadi Tabata Kisukuru, Dar es Salaam, ambapo ilitembelea The Community Centre for Preventive Medicine na kuwafikia wazee wanaoishi katika taasisi hiyo kwa msaada wenye lengo la kuboresha maisha yao ya kila siku.
Katika ziara hiyo, Meridianbet ilikabidhi msaada wa vyakula pamoja na vifaa vya usafi binafsi, hatua iliyolenga kupunguza changamoto zinazowakabili wazee hao. Miongoni mwa mahitaji yaliyowasilishwa ni mchele, sukari, mafuta ya kupikia, sabuni za unga na sabuni za vipande pamoja na vifaa mbalimbali vya usafi binafsi. Msaada huo una umuhimu mkubwa kwa taasisi hiyo kutokana na mahitaji makubwa yaliyopo, huku wazee wakihitaji mazingira safi, salama na chakula bora katika hatua hii ya maisha yao.
Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Afisa Mahusiano wa Meridianbet, Nancy Ingram, alisisitiza dhamira ya kampuni hiyo ya kuendelea kuwa sehemu ya jamii na kuwasaidia wale wanaohitaji. Alisema Meridianbet inatambua mchango mkubwa ambao wazee wameutoa katika kujenga jamii, hivyo ni muhimu kuwapa faraja na msaada pale wanapouhitaji. Kauli hiyo imekuja sambamba na matendo, kwani ziara hiyo haikuwa ya kukabidhi vifaa pekee, bali pia ilikuwa nafasi ya Meridianbet kusimama bega kwa bega na wazee hao na kuwapa muda wa kuzungumza nao.
Kwa upande wao, uongozi wa The Community Centre for Preventive Medicine ulieleza furaha yao baada ya kupokea msaada huo, wakisema Meridianbet imegusa moja kwa moja changamoto ya uhaba wa vyakula na vifaa vya usafi inayowakabili. Kwa taasisi inayohudumia kundi maalum kama wazee, msaada wa aina hii una nafasi kubwa katika kuimarisha huduma na ustawi wa wanaoishi hapo. Zaidi ya bidhaa zilizowasilishwa, ujumbe mkubwa uliobebwa na ziara hiyo ni kwamba jamii inapoungana, changamoto zinaweza kupunguzwa na watu wanaohitaji msaada wanaweza kupata matumaini mapya.
Kilichofanya ziara hiyo kuwa ya kipekee zaidi ni muda uliotumika pamoja na wazee hao. Wafanyakazi wa Meridianbet walishirikiana nao katika mazungumzo ya karibu, kucheka na kubadilishana mawazo, jambo lililogeuza makabidhiano hayo kuwa tukio la upendo na mshikamano. Hii ni sura nyingine ya Meridianbet inayoonyesha kuwa mafanikio yana maana zaidi yanapotumika kuleta furaha kwa wengine.



No comments:
Post a Comment