
Na Mwandishi Wetu
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule ameipongeza shule ya Green Acres ya jijini Dar es Salaam kwa kuwa ya kwanza kuanzisha klabu ya Uhamiaji.
Alitoa pongezi hizo akiwa shuleni hapo wakati akizindua klabu hiyo ambapo aliambatana na Afisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam, Vicent Haule na Meya wa Kinondoni, Songoro Mnyonge.
Mtambule alisema Wilaya yake inashule Zaidi ya 200 hivyo watapita shule baada ya shule kushawishi kuhakikisha kila shule inakuwa na klabu ya uhamiaji kama moja ya mbinu ya kuwafanya watoto wakatae uhamiaji haramu tangu wakiwa wadogo.
“Tutapita kuhamasisha shule zianzishe utaratibu huo ili wanafunzi wote wajue masuala ya uhamiaji wakiwa wadogo, tunapenda wahamiaji lakini wanaofuata taratibu na sharia za nchi yetu kwa hiyo lazima tuwajenge watoto kuchukua wahamiaji haramu tangu huku chini,” alisema
“Hata mama nyumbani anapotengeneza keki anatengeneza ili watoto wake wale sasa wakija watoto wa jirani wakila ile keki watoto wako wakakosa haipendezi, lazima tuwatolee taarifa kwa viongozi watu tunaoona kwamba ukaazi wao hapa nchini unamashaka mashaka,” alisema
Alisema Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ubungo itaibeba ajenda ya uhamiaji kama moja ya masuala nyeti kuhakikisha hakuna mtu anayeingia nchini na kukaa bila kufuata utaratibu kwenye wilaya hiyo.
“Kuna watu wanarubuniwa na vitu vidogo vidogo ili wawafiche hawa wahamiaji haramu, natoa wito tusithubutu kuwapa nafasi wahmiaji haramu kukaaa kwenye maeneo yetu kwasababu tukikubain umemficha tukamkamata nawewe utakakatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria,” alisema
DC alilishukuru Jeshi la Uhamiaji nchini chini ya Dk Anna Makakala kwa namna ambavyo limefanikiwa kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha linadhibiti wawhamiaji haramu.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge alisema kuanzishwa kwa klabu hiyo ni mafanikio makubwa sana kwani wanafunzi watakuwa na uwezo wa kufahamu madhara ya wahamiaji haramu tangu wakiwa wadogo.
“Nimuhimu sana kurithisha vijana hawa wadogo umuhimu wa kukataaa wahamiaji haramu kwasababu madhara yake yanajulikana, kuanzishwa kwa klabu hizi ni moja ya mambo ya msingi kabisa ya kupigiwa mfano,” alisema
“Nawapongeza Green Acres kwa uamuzi wa kukubali klabu hii kuzinduliwa hapa shuleni mmekuwa wa kwanza Mkoa wa Dar es Salaam, na kwa bahati nzuri shule hii iliasisiwa na mheshimiwa diwani wetu wa Magomeni Bujugo ambaye ametangulia mbele za haki lakini maono yake bado yanaishi,” alisema
Aidha, Meya Songoro alimpongeza Mkurugenzi wa shule ya Green Acres, Jackline Rushaigo kwa namna ambavyo amemudu kusimamia na kuendeleza maono ya baba yake kwa kuifanya shule hiyo kuendelea kuongoza kitaaluma.
Naye Mkurugenzi wa shule hiyo, Jackiline Rushaigo alilishukuru Jeshi la Uhamiani nchini kwa kuichagua shule hiyo kuwa ya kwanza kuanzisha klabu hiyo miongoni mwa maelfu ya shule zilizoko nchini.
“Mmeona namna tunavyolea vipaji vya wanafunzi wetu, tunajitahidi kuwalea kwenye maadili mem asana hata wanapokuwa nje ya shule wanakuwa watu wema sana na nawaahidi kuwa klabu hii itakuwa msaada mkubwa sana kwa taifa letu,” alisema
Alisema wameamua kuanzisha klabu hiyo hapo shuleni kama sehemu ya kuwajengea uzalendo wa kuipenda nchi yao na kukataa kuona watu wasio raia wakiishi nchini bila kufuata taratibu na sheria za nchi.


.jpeg)


.jpeg)

No comments:
Post a Comment