
LEO Julai 5, 2026, saa 23:00, Uwanja wa MetLife, New Jersey, utashuhudia pambano kali la michuano ya Dunia kati ya Brazil na Norway. Hii ni mechi ya Raundi ya 16 ambayo inaahidi burudani na mivutano mikubwa. Brazil, yenye mataji matano ya duniani, inatafuta kuvunja rekodi isiyofurahisha ya kutokuwahi kuishinda Norway katika pambano zima la kimataifa.
Kihistoria, Norway ni "kiboko" kwa Brazil, kwa kuwa katika michezo yote minne iliyopita, Brazil haijapata ushindi wowote. Tukio la kukumbukwa zaidi lilifanyika katika mashindano ya Dunia la 1998 huko Ufaransa, ambapo Norway iliibuka na ushindi wa 2-1 baada ya Brazil kuongoza kwa bao la Bebeto, na kufanikiwa kutinga hatua ya 16 Bora. Rekodi hii inawapa Norway imani kubwa, wakijua wana uwezo wa kuwapa taabu Wabrazil.
Kwa upande wa Brazil, chini ya ufundi wa Carlo Ancelotti, wanaingia mechi hii wakiwa na rekodi nzuri ya kutooshindwa katika mechi zao zote tatu za makundi na ushindi wa 2-1 dhidi ya Japan katika Raundi ya 32. Hata hivyo, wana wasiwasi wa jeraha la kiungo Lucas Paqueta, ambaye ni muhimu katika kuunda mashambulizi na kudhibiti mchezo wa kati.
Ancelotti anatarajiwa kubadilisha mbinu na kucheza kwa tahadhari zaidi, wakizingatia kuziba nafasi na kuzuia mashambulizi ya Norway, hasa wakipinga mipango ya kukabiliana haraka ya Norway na mchezaji wao hatari, Erling Haaland.
Ingia kwenye kasi ya kujishindia pesa kwenye michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Norway, wanaorejea kwenye michuano ya Dunia baada ya miaka 28, wamekuwa wakiendelea kuonyesha nguvu kubwa ya mashambulizi. Wao ni timu pekee ya Ulaya iliyofuzu kwa rekodi safi ya ushindi nane kwa nane katika mechi za kufuzu, wakifunga mabao 37.
Martin Odegaard ndiye kiungo anayeongoza mashambulizi, wakati Erling
Haaland akiwa na rekodi ya mabao 5 tayari katika michuano hii, anatarajiwa kuwa tishio kwa ulinzi wa Brazil, wakisaidiwa na winga mahiri Antonio Nusa. Jisajili sasa
Hivyo basi, mechi hii ya leo inakuja na uzito mkubwa wa kihistoria na mbinu. Brazil inatafuta kulipa kisasi na kuvunja ukame wa miaka 24 wa kutoshinda taji la Dunia, wakati Norway inatarajia kuendeleza rekodi yao ya kutowahi kushindwa na Brazil na kufanikisha safari yao ya kurudi katika hatua za juu za michuano. Hii ni mechi ambapo mkakati, uvumilivu, na uwezo wa kuzuia makosa makubwa ndio vitaamua.

No comments:
Post a Comment