HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 29, 2026

RC IRINGA ATETA NA VIONGOZI WA JUMUIYA ZA WAZEE MKOANI IRINGA

Mkuu wa mkoa wa Iringa Komred Kheri James,mapema leo amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Jumuiya za Wazee mkoani humo,lengo likiwa ni kupokea ushauri,Taarifa ya hali ya Jumuiya hizo pamoja na kushauriana juu ya masuala muhimu yanayo gusa mkoa wa Iringa.         

Akizungumza katika kikao hicho  Komred Kheri James amewashukuru Wazee wa mkoa wa Iringa kwa ushirikiano wao, busara,ushauri na ushiriki wao katika kujenga umoja,kusimamia maadili,kutoa ushauri na uzoefu,pamoja na utatuzi wa migogoro ya kijamii.                             

Aidha Komred Kheri James amewahakikishia Wazee wa mkoa wa Iringa dhamira ya Serikali kuendelea Kusimamia ustawi wa wazee,huduma kwa Wazee na kushirikiana na Jumuiya za Wazee zilizopo katika kuwahudumia na kusimamia maslahi na hoja za Wazee zinazo wasilishwa na kusimamiwa na Jumuiya hizo.










No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad