HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 7, 2026

OCTANT ENERGY KUENDELEA KUWEKEZA NCHINI KWA KUFUATA SHERIA

Na Mwandishi Wetu
RAIS  na Mkurugenzi Mkuu wa Octant Energy, Richard Schmitt, amesema Kampuni hiyo bado ina dhamira ya dhati kuendelea kuwekeza nchini kwa kuzingatia sheria viwango vya kitaalamu na maslahi ya wananchi.

Akizungumza katika banda la Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) kwenye Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba, Schmitt amesema kampuni hiyo inaendelea kutekeleza shughuli zake kwa kushirikiana kwa karibu na PURA pamoja na wadau wengine.

Akiwa katika banda la PURA, Schmitt amepata elimu kuhusu mfumo wa usimamizi wa shughuli za utafutaji, uendelezaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia nchini pamoja na kuhakikisha rasilimali za Petroli zinazoendelezwa zinazingatia sheria, na uwazi.

Octant Energy ni waendeshaji wa Kitalu cha Uchimbaji Tanga ambao wamefika katika banda la PURA kwenye maonesho ya Sabasaba kama moja ya wadau wa PURA. 



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad