HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 20, 2026

Jeshi la Polisi Wilaya ya Msoma yatoa msaada kwa watoto



Na Mwandishi Wetu
MKUU wa Polisi Wilaya ya Musoma mkoani Mara, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Edson Mwamafupa aliwaongoza Maafisa, Wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali katika zoezi la utoaji msaada kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Zoezi hilo la kibinadamu limefanyika katika Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Jipe Moyo kilichopo Manispaa ya Musoma, likiwa ni sehemu ya kuonyesha ukaribu na upendo wa jeshi hilo kwa jamii inayowazunguka.

Akikabidhi msaada huo wa vitu mbalimbali kwa msimamizi wa kituo hicho, Sister Maria Faustine, SSP Mwamafupa aliwataka watoto hao kutambua kuwa Jeshi la Polisi lipo pamoja nao wakati wote.

Aidha aliwasisitiza kuendelea kuzingatia masomo yao kwa bidii, wasaidiane na kupendana wao kwa wao, akibainisha kuwa tabasamu lao ndiyo furaha kuu ya jamii inayowazunguka.

Kwa niaba ya uongozi wa kituo na watoto wote, Sister Maria Faustine Alieleza kuwa ujio wa Jeshi la Polisi wilaya ya Musoma na msaada walioutoa si tu kwamba unasaidia kukidhi mahitaji ya watoto hao, bali pia unawapa faraja kubwa na kuwathibitishia kuwa jamii na vyombo vya ulinzi vinawajali na kuwalinda, huku akihitimisha kwa kuwaombea baraka za Mungu katika majukumu yao ya kila siku ya kulinda usalama wa raia na mali zao.




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad