HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 12, 2026

Watendaji wa Benki ya Absa Tanzania walivyoshiriki kikao cha Bajeti jijini Dodoma jana.

 


Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (katikati), akipozi kwa picha ya kumbukumbu na Ofisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Bernard Tesha (kushoto), na Mkuu wa Mikakati na Data wa benki hiyo, Bw. John Mosha, ndani ya viwanja vya bunge, mara baada ya mheshimiwa waziri, kuwasilisha bajeti ya serikali ya Sh 63.2 trilioni, itakayotumika katika Mwaka 2026/2027, bungeni, jijini Dodoma, jana.

Ofisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Bernard Tesha (kulia), Mkuu wa Mikakati na Data wa benki hiyo, Bw. John Mosha (wa tatu kulia), pamoja na baadhi ya wawakilishi kutoka taasisi za fedha, wakimsikiliza kwa makini, Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar, wakati akiwasilisha bajeti ya serikali ya Sh 63.2 trillioni, itakayotumika katika Mwaka 2026/2027, bungeni, jijini Dodoma, jana.

Ofisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Bernard Tesha (kulia, mstari wa nyuma) na Mkuu wa Mikakati na Data wa benki hiyo, Bw. John Mosha (wa tatu kulia, mstari wa nyuma), pamoja na baadhi ya wawakilishi kutoka taasisi za fedha, wakisimama kwa utambulisho, kabla Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar, hajawasilisha bajeti ya serikali ya Mwaka 2026/2027, bungeni, jijini Dodoma, jana.

Ofisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Bernard Tesha (wa tatu kushoto), akibadilishana mawazo na baadhi ya wawakilishi kutoka taasisi mbalimbali waliohudhuria uwasilishwaji wa bajeti ya serikali ya Mwaka 2026/2027, bungeni, jijini Dodoma, jana, uliofanywa na Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Air Tanzania Company Limited (ATCL) Mhandisi Peter Ulanga (Katikati), akipiga picha ya kumbukumbu na Ofisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Bernard Tesha (kulia kwake) na Mkuu wa Mikakati na Data wa benki hiyo, Bw. John Mosha, ndani ya viwanja vya bunge, muda mfupi baada ya Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar, kuwasilisha bajeti ya serikali ya Mwaka 2026/2027, bungeni, jijini Dodoma, jana.








No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad