HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, June 14, 2026

RC SHIGELLA AWATAKIA HERI WANANDOA, AKABIDHI GARI KAMA ZAWADI YA HARUSI

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigella, amemkabidhi zawadi ya gari aina ya Harrier,Bwana Harusi Buluguta Emmanuel Sagayika na kuwatakia wanandoa hao maisha mema ya ndoa yenye upendo, uvumilivu na kuheshimiana.

Akizungumza katika hafla hiyo, Shigella amesema ndoa imara hujengwa kwa misingi ya kuvumiliana, kusameheana na kushirikiana katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha. Amewasihi wanandoa hao kuendelea kuishi kwa upendo, mshikamano na maelewano ili kudumisha ndoa yao kwa muda mrefu.

Katika harusi hiyo, muimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini Tanzania, Martha Mwaipaja, alitoa burudani iliyoongeza shamrashamra na kuifanya hafla hiyo kuwa ya kipekee. Martha Mwaipaja alishiriki katika harusi ya mdogo wake, Diwani wa Kata ya Kalngalala,Ruben Sagayika,Buluguta Emmanuel Sagayika, iliyofanyika katika ukumbi wa Shule ya Wavulana ya Waja, wilayani Geita mkoani Geita.

Burudani hiyo iliwavutia wageni mbalimbali waliohudhuria harusi hiyo na kuungana katika kuwatakia kila la heri wanandoa hao wanapoanza maisha yao mapya ya ndoa.

Harusi hiyo ilihudhuriwa na mamia ya wageni pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM), akiwemo Meya wa Manispaa ya Geita, Leonard Bugomola, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Jumanne Misungwi, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Geita, Barnabas Mapande, na Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini, Chacha Wambura.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad