Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM — Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dkt. Dotto Kuhenga, amewapongeza Dkt. Frank Sanga na Dkt. Alex Benson baada ya kutunukiwa Shahada za Uzamivu (PhD) katika fani ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma, akieleza kuwa safari yao ni mfano wa uvumilivu, ustahimilivu na kujituma.
Dkt. Kuhenga alieleza hayo kupitia kurasa zake za kijamii akirejea tukio la Mei 25, 2026, ambapo wasomi hao walitunukiwa shahada hizo, akibainisha kuwa mafanikio yao ni ushuhuda kwamba juhudi na azma ya kufikia malengo huzaa matunda.
Akizungumzia uhusiano wake na Dkt. Frank Sanga, Dkt. Kuhenga alisema walifahamiana zaidi ya miaka 17 iliyopita katika Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, alipokuwa amejiunga kama mwandishi wa habari wa gazeti la The Citizen huku Dkt. Sanga akiwa Mhariri wa Mwanaspoti.
Alimuelezea Dkt. Sanga kuwa ni mtu mwenye upeo mkubwa wa kitaaluma, mwenye uzoefu mpana na mtazamo wa kimataifa katika tasnia ya habari.
Kuhusu Dkt. Alex Benson, alisema wamekuwa pamoja tangu walipokuwa wanafunzi wa shahada ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na baadaye wakawa wahadhiri wenza chuoni hapo pamoja na kushirikiana katika miradi mbalimbali ya kitaaluma.
Aidha, Dkt. Kuhenga alisema safari za masomo ya uzamivu za wasomi hao zinatoa funzo kwa wengi kuwa kujituma na kuwa na msimamo katika kufikia malengo ni msingi muhimu wa mafanikio.
Pia alibainisha kuwa Dkt. Frank Sanga na Dkt. Alex Benson walifanyiwa usimamizi wa tafiti na Profesa Michael Andindilile, ambaye pia aliwahi kuwa msimamizi wake katika safari yake ya shahada ya uzamivu miaka iliyopita.
“Maisha ni mzunguko wa aina yake. Hongereni sana Dkt. Frank Sanga na Dkt. Alex Benson. Simulizi zenu ni chachu kwa wengi,” ameandika Dkt. Kuhenga.

No comments:
Post a Comment