HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, April 24, 2026

WASHIRIKI JUMA LA ELIMU 2026 WATEMBELEA SHULE MBALIMBALI WILAYANI MOMBA

 

Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bi. Martha Makala akilakiwa na Wanafunzi wa Shule ya wasichana ya Songwe, wilayani Momba alipofanya ziara katika shule hiyo pamoja na washiriki wa Juma la Elimu Kitaifa linalofanyika Mkoani Songwe ambapo wadau mbalimbali wa Elimu nchini wanashiriki.


Wadau mbalimbali wa elimu wakiwa katika mikutano na Wanafunzi wa baadhi ya Shule za wilayani Momba, ambapo maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanafanyika.

Wadau mbalimbali wa elimu wanaoshiriki maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanafanyika, Wilayani Momba Mkoa wa Songwe.

Wadau mbalimbali wa elimu na washiriki wa maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanafanyika, Wilayani Momba Mkoa wa Songwe wakiwa katika ziara kutembelea shule na kuzungumza na wanafunzi na wazazi wa maeneo hayo.

Wadau mbalimbali wa elimu na washiriki wa maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanafanyika, Wilayani Momba Mkoa wa Songwe wakiwa katika ziara kutembelea shule na kuzungumza na wanafunzi na wazazi wa maeneo hayo.

Wanafunzi wa Shule ya wasichana ya Songwe (kulia), Wilayani Momba wakimkabidhi risala Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bi. Martha Makala alipotembelea shule hiyo pamoja na wadau wa elimu wanaoshiriki maadhimisho ya Juma la Elimu GAWE 2026 mkoani Songwe.

Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bi. Martha Makala akizungumza na Wanafunzi, wazazi na wadau wengine wa elimu katika Shule ya Wasichana ya Songwe, wilayani Momba alipofanya ziara katika shule hiyo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa, GAWE 2026.

Wanafunzi wakitoa burudani kwa wadau wa elimu walipotembelea shuleni hapo.

Mikutano ya wadau wa elimu na wanafunzi na wazazi ikiendelea kwenye Maadhimisho ya Juma la Elimu.

Wadau mbalimbali wa elimu wakiwa katika mikutano na Wanafunzi wa baadhi ya Shule za wilayani Momba, ambapo maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanafanyika.

Wadau mbalimbali wa elimu wakiwa katika mikutano na Wanafunzi wa baadhi ya Shule za wilayani Momba, ambapo maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa yanafanyika.

MAADHIMISHO ya Juma la Elimu Kitaifa yanaendelea Mkoani Songwe ambapo TEN/MET na wadau wa Elimu nchini wametembelea shule ya wasichana ya Songwe, Wilayani Momba. Shule hiyo iliyoanza na wanafunzi 25 chini ya usimamizi wa mkoa, sasa imekua hadi kufikia idadi ya wanafunzi 161 na walimu 15 wenye dhamira thabiti ya kuinua elimu ya mtoto wa kike.

Akizungumza na wadau wa elimu, Mkuu wa Shule Bi. Janeth Mwamwile amesema kuwa kwa miaka minne mfululizo shule imepata ufaulu wa asilimia 100, na hivyo kung’ara katika ngazi ya wilaya, mkoa na hata taifa. Lakini pamoja na mafanikio hayo, amebainisha shule bado inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo za miundombinu kama nyumba za walimu, maabara, bwalo la chakula, mabweni, jengo la utawala, jiko hivyo kutoa wito kwa wadau wa sekta ya elimu kuwashika mkono ili kuchochea mafanikio hayo.

Kwa upande wa Mtandao wa Elimu Tanzania @tenmet Bi. Martha Makala, Mratibu wa Mtandao), amesisitiza umuhimu wa kusaidia wasichana ili waweze kutimiza ndoto zao akitolea mfano wa Elimu yake aliyoipata kutoka shule ya wasichana kama chachu ya kufanikiwa maishani. Aidha, Bi. Makala ameahidi kuwa changamoto zilizobainishwa zimepokelewa na zitachakatwa ili kuona namna wadau wa TEN/MET wanavyoweza kushirikiana katika utatuzi wake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad