HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 2, 2026

TIRDO YAWAALIKA WADAU WA NGOZI KUPATA UTAALAM WA UZALISHAJI BORA

Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) imewaalika wadau wa ngozi nchini kupata mafunzo juu ya uchakataji na utengenezaji bidhaa za ngozi nchini .

Hayo yameelezwa na Kaimu Mkurugenzi wa TIRDO Mhandisi Ramson Mwilangali wakati akifunga mafunzo ya siku tano kwa wanafunzi na wazalishaji wa Bidhaa za ngozi nchini .

Mafunzo hayo ya siku tano yamelenga kuwajengea uwezo wazalishaji wa ngozi kutoka mikoa ya Pwani , Morogoro,Dar es salaam na Kilimanjaro lengo likiwa ni kuhakikisha ngozi inayozalishwa hapa nchini inachakatwa na kuzalisha bidhaa tofauti na sasa ambapo kwa kiasi kikubwa ngozi inauzwa nje ya nchi kabla ya kuchakatwa .

Mhandisi Ramso amesema kuwa soko la Tanzania inahitaji zaidi ya jozi ya viatu milioni 54 huku Viwanda vya ndani vikizalisha jozi elfu tatu tu ambayo ni chini ya asilimia kumi ya mahitaji bidhaa hiyo kwa mwaka.

"Tunalenga kuongeza uzalishaji wa ndani kufikia asilimia 50 ya mahitaji ya nchi ili kuziba pengo linaloagizwa kutoka nje .

Kwa upande wa mtaalam ngozi wa na nguo kutoka TIRDO Mhandisi Yusufu Sampuli amesema kuwa lengo lilikuwa ni kutoka mafunzo kwa watu 15 lakini kutokana na uhitaji wamefika watu 28 kutoka mikoa hiyo mitano . "Tumepokea wanufaika wa mafunzo haya waliopo katika hatua mbali mbali ,wengine wamewahi kuzalisha viatu ,wengine ni mara yao ya kwanza lakini Kila Mmoja ametoka hapa na utaalam wa kutosha juu ya hatua za uzalishaji na utambuzi wa ubora wa ngozi aliongeza Mhandisi Sampuli.

Mafunzo hayo yametoleaa kwa wazalishaji wa bidhaa kama viatu, mabegi ,mikanda nk kwa wamiliki wa viwanda vidogo pamoja na wajasiriamali wadogo na wakubwa juu ya elimu ya uboreshaji bidhaa za ngozi.

Baadhi ya wanufaika wa mafunzo hayo Bi.Yusra Omary Ally Kutoka Dar es salaam , Ndugu Piscus Maresh kutoka Pwani na Bi Pauline Kawa wameshukuru Kwa mafunzo hayo na kuishukuru TIRDO Kwa kuwapa nafasi ya kujifunza.

Mmoja wa washiriki hao Bi Yusra Omary amesema kuwa ni mara yake ya kwanza kupata mafunzo hayo lakini ndani ya siku nne ameweza kutengeneza kiatu kwa hatua ya kwanza ya kupima ngozi, kukata hadi kukamilika kabisa. "Mimi siku zote nilikuwa na wazo lakini sikujua nianzie wapi ,kupitia mafunzo haya Sasa naweza kutengeneza kiatu katika hatua zote aliongeza Bi Yusra.

Mafunzo hayo yamedhaminiwa na Wizara ya Viwanda na Biashara , Jumuhia ya Umoja wa Ulaya ,Jumuhia ya Afrika Mashariki pamoja na kituo Cha Biashara cha Kimataifa (ITC ) chini ya mradi wake wa MARKUP II inayolenga kusaidia uzalishaji wa Bidhaa Bora za ngozi barani Afrika .

Wataalam kutoka TIRDO walioshiriki katika kufanikisha mafunzo hayo kwa vitendo Mhandisi Yusufu Sampuli, Kenan Tarimo , Paul Kimathi pamoja na Innocent Barongo ambao kwa pamoja wametoa wito kwa wanufaika hao wa mafunzo kutosita kuwasiliana nao pamoja na kufika TIRDO kupata ushauri wa kitaalam pamoja na upimaji wa Kimaabara.









No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad