Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB,Mkurugenzi wa Tehama wa Benki hiyo,Edward Mpina amekabidhi madarasa mawili waliojengwa na udhamini wa Benki hiyo ya CRDB katika Shule ya Msingi ya Fulwe pamoja na madawati 30 kwa Mbunge wa Jimbo la Geita,Joseph Musukuma.
Akizungumza wakati wa kukabidhi madarasa hayo pamoja na madawati 30 Halmashauri ya wilaya ya Geita,Mpina amesema dhumuni ya benki hiyo ni kuona wanafunzi wanakaa vizuri darasa kwa nafasi ili waweze kusoma vizuri na kuandika na kuinua ufaulu wao shuleni.
“Dhamira ya dhati ya Benki ya CRDB ni kushirikiana na jamii katika kuleta maendeleo pia inathibitisha kuwa tunaamini katika nguvu ya jamii kama msingi wa maendeleo endelevu katika miongo mitatu iliyopita tunajivunia kwa kupitia sera ya uwekezaji kwa jamii kwani tumefanikisha miradi mbalimbali na ujenzi wa madarasa hayo imegharimu Shilingi Milioni 50” amesema Mpina.
“CRDB ina maeneo mengi inayotekeleza miradi ya maendeleo lakini leo inaandikwa historia katika jimbo langu lakini napendekeza mimi na familia yangu na baadhi ya wadau tutatoa shilingi Milioni 50 kwa ajili ya madarasa mengine mawili kutokana na mkandarasi aliyejenga amenishawishi kujenga pia kutokana na fedha iliyotumika inaendana na ubora wa madarasa” amesema Mbunge Musukuma.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi,Leonard Kamata amesema shule hiyo ilianzishwa enzi za ukoloni mwaka 1956 ambapo kwa mwaka huu shule hiyo ina wanafunzi 695,wavulana 330 na wasichana 365 na vyumba vya madarasa 16 na amesema uwepo wa madarasa hayo utapunguza msongamano wa wanafunzi darasani.














No comments:
Post a Comment