
Na Khadija Kalili
BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha limepitisha bajeti ya Mil. 50 kwa kila Kata zitakazotumika kwa ajili ya kufungua barabara zillizoharibika na kukarabati miundombinu ya barabara zilizoharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha.
Fedha hizo zimepitishwa kufuatia kikao cha kikanuni na Baraza hilo lililofanyika tarehe 14, 2026 ambapo utekelezaji wake ni katika kipindi cha mwaka wa fedha 2026-2027.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kibaha Dkt. Mawazo Nicas amesema kuwa awali fedha hizo zilitengwa kiasi cha Mil.30 kwa kila Kata lakini kutokana na kubaini ubovu wa barabara hizo wamelazimika kuongeza bajeti hiyo hadi kufikia Mi.50.
"Tunatambua kwamba Manispaa ya Kibaha kuna Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) Pamoja na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS )
lakini Manispaa tumeona ni vema kutoa fedha hizo na kuzifungua baadhi ya barabara kwa dharula ili kupunguza changamoto ya ubovu wa barabara.
Mstahiki Meya Dkt.Nicas amezitaja Kata 14 zitakazopata Mi.50 kuwa ni Mailimoja, Tumbi,Pangani, Picha ya Ndege,Kongowe, Mkuza na Tangini.
Kata zingine ni Viziwaziwa, Msangani, Kibaha,Mbwawa,Visiga,Misugusugu na Tumbi.

Dkt.Nicas amewapongeza madiwani wa Manispaa hiyo kwa kuridhia bajeti hiyo inayokwenda kutatua kero ya barabara kadhalika amempongeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Kibaha Dkt.Rogers Shemwelekwa kwa kazi nzuri ya kukusanya mapato ambayo yanasaidia kutatua kero za wananchi.
"Wananchi wetu kilio chao kikubwa ni miundombinu barabara hizi zipo chini ya TARURA na TANROADS lakini kwa upendo wa Wataalamu na Madiwani kuwajali wananchi wake wameamua kutenga fedha hizo ambazo ni mapato ya ndani zikatumike kurekebisha maeneo korofi", amesema.
Diwani wa Kata ya Sofu Mashaka Mahande amesema kutengwa kwa fedha hizo kunakwenda kupunguza kero ya barabara ambazo nyingi zimeharibika zaidi kipindi cha mvua.


No comments:
Post a Comment