HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, March 14, 2026

TASAC Yapata Pongezi kwa Kuandaa Iftar na Kuwajumuisha Watoto Yatima

 

Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa  akizungumza katika Iftar iliyoandaliwa na TASAC  kwa kushirikisha watoto ya Yatima wa Kituo cha Hisani Kigamboni iliyofanyika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere JNCC jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Mohamed Salum akitoa maelezo kuhusiana na TASAC  kuandaa Iftar   kwa kushirikisha watoto ya Yatima wa Kituo cha Hisani Kigamboni iliyofanyika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere JNCC jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya TASAC Nahodha Mussa Mandia akitoa akizungumza katika Iftar iliyoandaliwa na TASAC  kwa kushirikisha watoto ya Yatima wa Kituo cha Hisani Kigamboni iliyofanyika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere JNCC jijini Dar es Salaam.



Picha mbalimbali za zawadi  kwa Kituo cha Watoto Yatima cha Hisani Kigamboni.
Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa  akiwa na meza kuu katika picha ya pamoja na Menejimenti ya TASAC mara baada  ya Iftar iliyoandaliwa na TASAC  kwa kushirikisha watoto ya Yatima wa Kituo cha Hisani Kigamboni iliyofanyika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere JNCC jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu
WAZIRI  wa Uchukuzi, Makame Mbarawa, amelipongeza Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kwa kuandaa hafla ya Iftar iliyowakutanisha wadau wa sekta ya usafiri majini pamoja na watoto yatima hatua inaongeza mshikamano na kuimarisha ushirikiano katika sekta hiyo.

Waziri Mbarawa ameyasema hayo katika hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Convention Centre jijini Dar es Salaam

Profesa Mbarawa alisema hatua ya TASAC kuwakutanisha wadau katika futari ya pamoja inalenga kudumisha urafiki, mshikamano na umoja miongoni mwa wadau wa sekta ya usafirishaji majini.

Amesema Mwezi Mtukufu wa Ramadan hufundisha jamii kujenga mahusiano mema na kuimarisha mshikamano, jambo ambalo TASAC imelidhihirisha kwa vitendo kupitia hafla hiyo ya iftar.

“Katika sekta ya usafiri majini, mshikamano na ushirikiano kati ya serikali, Taasisi na Wadau wa sekta binafsi ni jambo muhimu katika kuhakikisha sekta hii inaendelea kukua na kuchangia maendeleo ya uchumi wa taifa,”amesema.

Profesa Mbarawa pia alitambua mchango wa TASAC katika kusimamia na kudhibiti usafiri majini nchini, akieleza kuwa taasisi hiyo ina jukumu kubwa la kuhakikisha usalama wa vyombo vya majini, abiria na mali zao pamoja na kudhibiti uchafuzi wa mazingira katika bahari na maziwa unaotokana na shughuli za meli.

Alifafanua kuwa TASAC pia inasimamia usajili wa meli, kudhibiti huduma za usafiri majini ikiwemo bandari na huduma za uwakala wa meli pamoja na kuhakikisha sheria na kanuni za kimataifa za usafiri majini zinafuatwa ipasavyo.

Aidha, amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuweka mkazo katika kuimarisha miundombinu ya uchukuzi ili kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi.

Amesema katika sekta ya usafiri majini, serikali imechukua hatua mbalimbali za kuboresha bandari na kuimarisha usalama wa vyombo vya majini ili kuhakikisha wananchi na mali zao zinalindwa.

“Serikali imejidhatiti kuhakikisha wananchi na mali zao wanakuwa salama kwa kuimarisha mifumo ya uokozi ili hata panapotokea dharura uwepo wa msaada wa haraka,” alisema.

Kutokana na hilo, Waziri Mbarawa alitoa wito kwa wadau wa sekta ya usafiri majini kuendelea kushirikiana kwa karibu na TASAC kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zote zinazosimamia shughuli za usafiri majini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Mohamed Salum, alisisitiza umuhimu wa umoja na mshikamano miongoni mwa wadau na wafanyakazi wa taasisi hiyo.

Alisema kukutana pamoja katika mwezi wa Ramadanini fursa nzuri ya kusherehekea mafanikio ya kazi yaliyofikiwa na TASAC pamoja na kutathmini hatua zilizopigwa katika kuboresha huduma za taasisi hiyo.

“Kukutana pamoja katika mwezi huu ni fursa ya kujivunia mafanikio yaliyopatikana kupitia juhudi za pamoja za wafanyakazi na wadau wetu, huku tukizidi kuimarisha mshikamano na ushirikiano,” alisema.

Katika hafla hiyo iliyowashirikisha watoto yatima kutoka Kituo cha Hisani Kigamboni kwa kuwapatia chakula cha iftar pamoja na mahitaji mbalimbali muhimu kwa ajili ya mfungo wa Ramadhani na maandalizi ya sikukuu ya Eid.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad