HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 9, 2026

TADB Yawafariji Watoto 130 Wenye Mahitaji Maalum Zanzibar Katika Mfungo wa Ramadhani

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) leo Machi 9, 2026 imetembelea watoto wenye mahitaji maalum katika vituo viwili vya kulelea watoto Zanzibar kwa lengo la kuwafariji na kuwaunga mkono katika kipindi hiki cha mfungo mtukufu wa Ramadhani.

Katika ziara hiyo, benki ilifika katika Kituo cha ZASO Children Home kilichopo Fuoni Mambo Sasa ambacho kina watoto 47, pamoja na Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Mssers Markaz Orphanage kilichopo Fuoni Jitimai chenye watoto 83.

Kupitia ziara hiyo, TADB ilikabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali muhimu kwa watoto hao ili kuwasaidia katika maisha yao ya kila siku, hususan katika kipindi hiki cha Ramadhani.

Msaada huo ulikabidhiwa rasmi na Meneja wa Kanda ya Zanzibar wa TADB, Bw. Ally Jamal, akiongozana na wafanyakazi wa benki hiyo.

Hatua hiyo inaashiria dhamira ya TADB ya kuendelea kushiriki katika shughuli za kijamii, kuonesha upendo na mshikamano, pamoja na kugusa maisha ya makundi yenye uhitaji maalum katika jamii.














No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad