Hatua hiyo imekuja mara baada ya NEMC kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu utiririshaji wa majitaka kwenye Mazingira hali iliyozua taharuki kwa afya za wananchi wanaozunguka eneo hilo.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Idara ya Uzingatiaji na Utekelezaji wa Sheria (NEMC) Bi. Luhuvilo Mwamila amesema awali NEMC ilifanya ukaguzi na kubaini mtambo wa kutibu majitaka usiotumika badala yake, kiwanda kimekuwa kikitiririsha maji taka yasiyotibiwa moja kwa moja kwenye mazingira na kumwaga tope lenye kemikali hatarishi (sludge).
Uchunguzi zaidi umeonyesha kuwa kiwanda kimekuwa kikinyonya majitaka na kuyamwaga kwenye machimbo ya mchanga nje ya eneo lao, huku tope sumu wakilichoma katika maeneo hayo hayo.
Hali hii ni kinyume cha taratibu za mazingira na kuhatarisha afya ya jamii na usalama wa ikolojia. kutotii maelekezo ya mamlaka, hatua kali zimechukuliwa ili kulinda mazingira na afya ya wananchi.







No comments:
Post a Comment