HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, February 14, 2026

TAB Kinondoni Yapokea Msaada wa Fimbo kutoka Meridianbet

 

MERIDIANBET Tanzania imeendeleza dhamira yake ya kurudisha kwa jamii kwa kutoa msaada wa fimbo maalum za kutembelea (walking canes) kwa watu wasioona jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo ya kijamii ilifanyika katika ofisi za Tanzania Association of the Blind (T.A.B) zilizopo Kinondoni, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) ya kampuni hiyo.

Tukio hilo lilihudhuriwa na Mwenyekiti wa T.A.B pamoja na wanachama wa chama hicho, huku Meridianbet ikiwakilishwa na timu yake iliyoongozwa na Afisa Uhusiano wa Umma, Nancy Ingram. Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Nancy Ingram alisisitiza kuwa msaada huo ni ishara ya mshikamano na upendo kwa watu wenye ulemavu, na ni sehemu ya maadili ya kampuni kuunga mkono makundi yenye mahitaji maalum katika jamii.

Meridianbet haikuachi nyuma, kuna michezo mbalimbali ya kasino mtandaoni pamoja na mechi za kimataifa za kubashiri zenye odds bomba zinazokuongezea nafasi ya kuongeza kipato chako kila siku. Kujiunga ni rahisi, Tembelea meridianbet.co.tz au piga *149*10#.

Mwenyekiti wa T.A.B aliishukuru Meridianbet kwa msaada huo, akieleza kuwa fimbo hizo zitasaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha harakati za kila siku za watu wasioona, na kuongeza usalama na uhuru wao wanapotembea katika mazingira mbalimbali. Alibainisha kuwa ushirikiano kati ya taasisi binafsi na mashirika ya kijamii una mchango mkubwa katika kuboresha maisha ya watu wenye ulemavu.

Meridianbet imekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza miradi mbalimbali ya kijamii inayolenga kusaidia makundi yenye uhitaji, hususan watu wenye ulemavu. Kupitia mpango huu, kampuni imeonesha kwa vitendo kuwa inaamini katika kujenga jamii jumuishi inayotoa fursa sawa kwa wote bila kujali changamoto walizonazo.

Kwa ujumla, msaada huu wa fimbo za kutembelea ni kielelezo cha dhamira thabiti ya Meridianbet ya kuchangia maendeleo ya jamii na kuimarisha ustawi wa watu wenye ulemavu. Kampuni hiyo imeahidi kuendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali za kijamii katika kuleta mabadiliko chanya na kuendeleza misingi yake ya kutoa mchango kwa jamii kila inapopata fursa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad