Muuzaji wa mishikaki jijini Dar es Salaam, Bakari Hamisi Bakari, ameanza safari mpya ya kiuchumi baada ya kujishindia boda boda kupitia droo ya kwanza ya kampeni ya #ShindaBoda inayoendeshwa na PigaBet. Ushindi huo unatajwa kuwa chachu ya mabadiliko kwake, akisema utamwezesha kuongeza kipato, kuimarisha mtaji wa biashara yake na kufungua milango ya kupanua shughuli zake zaidi ya kuuza mishikaki.Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa zawadi yake, Bakari alisema boda boda hiyo itampa fursa ya kujipanga upya kiuchumi kwa kuunganisha biashara yake ya sasa na huduma za usafiri, jambo analoamini litamsaidia kufikia ndoto yake ya kuwa mfanyabiashara mkubwa. Alisisitiza kuwa ushindi huo si bahati tu bali ni mwanzo wa safari ya kujikwamua kimaisha na kujenga mustakabali imara.
Katika hafla hiyo, mshindi mwingine wa droo ya kwanza, Chirag Narsana, naye alipokea boda boda yake akisema itarahisisha shughuli zake za kila siku na matumizi binafsi. Kampeni ya “Shinda Boda – Kuwa Boss Kila Wiki” inalenga kuwapa Watanzania fursa ya kujiongezea kipato, huku waandaaji wakikumbusha umuhimu wa kucheza kwa uwajibikaji kwa kuzingatia umri wa miaka 18 na kuendelea.

.jpeg)
No comments:
Post a Comment