Na Mwandishi Wetu
MKUU wa Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Shaibu Ndemanga amewashauri wakutubi kuhifadhi na kulinda taarifa na kumbukumbu za taifa lao hasa kwa kuzingatia taaluma yao ni muhimu katika ulimwengu wa sasa.
Ametoa ushauri huo alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 31 ya Chuo cha Ukutubi na uhifadhi Nyaraka (SLADS) yaliyofanyika wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani ambapo takribani wanafunzi 135 wamehitimu stashahada ya Ukutubi na Uhifadhi Nyaraka.
Ndemanga amesema katika ulimwengu wa sasa ambapo teknolojia imeendelea kukua kwa kasi Mkutubi ni mtu muhimu katika kuwa mlinzi wa taarifa na kumbukumbu.“Mmebeba mzigo mzito na naamini mtaenda kuitendea haki taaluma yenu.”
Pamoja na ushauri huo kwa wahitimu hao pia ameiomba sekta ya elimu nchini kuangalia upya mitaala na Sera ya elimu ili kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa wakutubi.
Aidha amesisitiza kwamba umekuwepo uhitaji wa Wakutubi katika maktaba za shule za Msingi, Sekondari na Vyuo vya Amali.
“Sehemu ya fedha hizo zimeanza kutumika kuboresha miundombinu ya Chuo.Pia nitoe ombi kwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Bogamoyo kuwezesha wanafunzi wa SLADS kupata nafasi za kufanya mafunzo kwa vitendo katika Wilaya hii.”
Wakati huo huo hiyo Mwakilishi wa Kamishna wa Elimu, Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia anayeshughulikia Masuala ya Maktaba na Kiswahili, Dkt. Maryam Mwinyi, amewaomba wahitimu hao kutumia elimu waliyoipata kuitumia kwa maendeleo na wasiitumie vibaya kwenda kubomoa taifa.

No comments:
Post a Comment