HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 5, 2025

MZAWA APONGEZWA NA MWENGE WA UHURU KWA KUJENGA KITUO CHA AFYA YA SHILINGI BILIONI TATU - MBOGWE DC

Wananchi wanaowekeza kwenye sekta mbalimbali ikiwemo afya na elimu wametakiwa kulipa kipaumbele suala la uzalendo ili miradi yao isiwe kibiashara zaidi na iwe sehemu ya huduma za kijamii.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mwaka 2025, Ismail Ali Ussi alitoa maelekezo hayo jana akiwa wilayani Mbogwe mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika Kituo cha Afya binafsi cha Gakala.

Ussi alitaja kituo cha afya Gakuli kuwa ni miongoni mwa uwekezaji wa mfano kwani mmiliki ametoa fursa kubwa ya ajira kwa vijana wa kitanzania ambao wamebobea kwenye fani na taaluma mbalimbali.

Ussi alitaja kituo cha afya Gakuli kuwa ni miongoni mwa uwekezaji wa mfano kwani mmiliki ametoa fursa kubwa ya ajira kwa vijana wa kitanzania ambao wamebobea kwenye fani na taaluma mbalimbali.

“Leo hii vijana wetu waliosomea fani za udaktari uhudumu, kukaribisha wageni, fani za usafi, wamepata ajira katika eneo hili, na hakuna mtu anayetoka nje ya Tanzania ambaye ameajiriwa katika hospitali hii.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Afya Gakala katika kata ya Bukandwe, Bunga Dadu alisema mradi una thamani ya Sh. Bilioni 3 na mpaka sasa kiasi cha Sh. Milioni 539 zimetumika kwa awamu ya kwanza.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad