Na Mwandishi wetu
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Watumishi Housing Investment (WHI), AbdulRazak Badru ametoa wito kwa watumishi wa Umma kuchangamkia fursa ya uwekezaji kupitia dirisha E-Wekeza linalotarajiwa kuzinduliwa na serikali kupitia mfumo wa watumishi portal hivi karibuni. 
Badru ameyasema hayo wakati akizungumza na wawekezaji na wajumbe wa bodi katika Mkutano Mkuu wa pili wa Mfuko wa Uwekezaji wa Faida 2025 ujulikanao kama Faida Fund. Badru Pia ameiomba Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuhimiza na kuwakumbusha watumishi wa umma kushiriki katika kuwekeza kwa mwendelezo ili kujiwekea akiba kidogo kidogo Kwa manufaa yao ya Sasa na baadae.


No comments:
Post a Comment