Kamishna wa Kamisheni ya Polisi Jamii (CP) Faustine Shilogile amesema hayo wakati akihitimisha mkutano wa mafunzo yaliyotolewa kwa wananchi wa wilaya ya Geita kwa siku 14 ambapo wametembelea Kata 6 na vijiji 11.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita,Safia Jongo amesema uhalifu unaotokea sehemu mbalimbali inatokana na malezi hasa vibaka chanzo kikubwa na wazazi wanaona jukumu la ulezi ni la askari wa jeshi la polisi au serikali.
‘Mafunzo yaliyotolewa kwa wananchi wa wilaya ya Geita na kusikiliza kero zao nimeona juhudi za haraka zinahitajika kuzunguka kata zote kusikiliza kero za wananchi zinazohusiana na usalama na kuzitatua.’amesema Jongo
Kampeni ya Siku 14 ya kufikisha elimu ya ulinzi shirikishi Mkoani Geita iliyoratibiwa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Kampuni ya Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML) imehitimishwa na Kamanda wa Kamisheni ya Polisi Jamii (CP) Faustine Shigolile katika kata ya Nyarugusu iliyopo halmashauri ya wilaya ya Geita.
No comments:
Post a Comment