HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 17, 2025

POLISI TANZANIA YAJIPANGA KULIPA 'KISASI' KWA MBEYA CITY BABATI, MANYARA

TIMU ya Polisi Tanzania Ijumaa hii Aprili 18, 2025 inawakaribisha Mbeya City katika mchezo wa Ligi ya Championship, mchezo utakaochezwa katika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa Mjini Babati.

Afisa habari wa timu ya Polisi Tanzania Inspekta Frank Lukwaro amesema alama tatu za mchezo huo ni muhimu ikiwemo kulipa kisasi cha kufungwa na Mbeya City katika mchezo wa duru la kwanza katika Uwanja wa Sokoine Mbeya hivyo wameupa umuhimu mkubwa.

Alisema mpaka sasa kikosi hicho kipo vizuri na hakuna majeruhi hivyo kilichobaki ni kuhakikisha kila mchezaji anapambana kuhakikisha wanapata ushindi.

Lukwaro ametoa wito kwa  mashabiki wa timu hiyo mjini Babati  kujitokeza kwa wingi ili kushirikiana kwa kuwa itakuwa siku ya mapumziko.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad