Katika ziara hiyo, wametoa msaada wa bidhaa mbalimbali, ikiwemo chakula vikiwa na thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 1.7 kwa ajili ya watoto 65 wanaolelewa kituoni hapo.
Sr. Hellen, mlezi wa kituo, ameishukuru TEA kwa mchango wao, akisema kuwa kituo hicho hutegemea misaada ya wadau ili kuhudumia watoto wake.
Meneja wa Rasilimali Watu na Utawala wa TEA, Bi. Alice Lukindo, amesema wanawake wa TEA wameamua kusherehekea siku hii kwa kuleta faraja kwa watoto. "Wanawake tuna wajibu wa kutunza familia na jamii. Leo tumeamua kugusa maisha ya watoto hawa."
✨ Kuadhimisha ni kufanya matendo mema! ✨



No comments:
Post a Comment