HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, March 15, 2025

VIFO VYA UKATILI VYAPUNGUA KWA ASILIMIA 81 GEITA - RPC SAFIA JONGO

Mkoa wa Geita umefanikiwa kupunguza vifo vya wanawake vitokanavyo na matukio ya ukatili kwa asilimia 81 ndani ya mwaka mmoja kutoka vifo 37 mwaka 2023 hadi matukio ya vifo saba mwaka 2024.

Aidha Matukio ya ukatili wa kijinsia mkoani Geita yamepungua kwa asilimia 44 ndani ya kipindi hicho kutoka matukio ya ukatili 95 yaliyoripotiwa mwaka 2023 hadi matukio 53 yaliyoripotiwa mwaka 2024.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Safia Jongo amesema hayo katika sherehe maalum za Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania mkoa wa Geita.

Kamanda Jongo amesema hayo ni matokeo ya elimu na ulinzi na usalama kwa ushirikiano kati ya jeshi la polisi ikiwemo mtandao wa polisi wanawake, polisi jamii pamoja na viongozi mbalimbali wa kijamii.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Geita, Martine Shigella amepongeza juhudi za jeshi la polisi mkoani Geita na kukiri kuwa wakati anawasili mkoani Geita  kulikuwa na matukio mengi tofauti na sasa ambapo usalama umeimarika katika jamii yote.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad