HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 6, 2025

ORYX YAMWAGA FUTARI KWA RAMADHAN NA KWARESMA

 




*Ni kwa wateja watakao jaza gesi katika kipindi cha mfungo

Na Mwandishi Wetu

Kampuni ya Oryx yashusha neema katika mwezi mtukufu wa Ramadhan na Kwaresma kwa wateja wake wataojaza gesi ya majumbani kupata zawadi ya futari ya Tambi ,Sukari pamoja maziwa ya Nazi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Oryx  Futari Kunoga ya Mkuu wa Idara ya Mauzo na Masoko wa Oryx Shaban Fundi amesema kampuni hiyo inafanya utoaji wa futari kwa mifungo ya Ramadhan na Kwaresma ikiwa ni kurudisha kwa jamii.

Amesema kuwa zawadi hizo ni nchi zima kwenye maduka ya kampuni ya Oryx pamoja na maduka mengine yaliyodhibitishwa.

"Tumejipanga kuwafikia wateja wetu katika kipindi hiki kupata zawadi ya futari pindi watakavyojaza gesi kuanzia kilogram sita na kuendelea na neema hii sio ya kukosa"amesema Fundi.

Aidha amesema kuwa zawadi ya  Futari ni kwa kipindi hiki cha mifungo miwili na hakuna mtu atakaye jaza gesi ya kupikia majumbani akakosa zawadi hizo.

Fundi amesema kuwa uhamasishaji wa matumizi ya Nishati safi ya Kupikia Oryx inaendelea ikiwa ni kuwafikia watanzania wote ili kufikia lengo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad