HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 25, 2025

HODI CHUMBAGENI

 Katika kuendelea kutoa elimu juu ya Taaluma ya Uhasibu kwa Shule za sekondari na vyuo nchini Tanzania Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania(NBAA) imepiga hodi ya Shule ya Sekondari ya Chumbageni ili kuwapa elimu hiyo

Akizungumza wakati wa utoaji wa elimu shuleni hapo, mfanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Sawa Ngendabanka  amewataka wanafunzi kuzingatia masomo ya hesabu na kiingereza kwani ndio msingi wa taaluma ya Uhasibu.

Naye Afisa Masoko na Mawasiliano Mwandamizi wa NBAA, Magreth Kageya amesema kwasasa NBAA inatoa kozi nyingine za muda mfupi kama vile Cheti na Diploma ya IPSAS pamoja na "Professional Diploma in Internal Auditing - PDIA" kozi ambayo inatoa misingi kwa mtu yeyote anayefanya au anatamani kufanya kazi za ukaguzi wa ndani.

Pia amesema si kila aliyesomea uhasibu anaweza kufanya kazi za kihasibu bali inabidi kufanya mitihani ya Bodi hiyo ili kupewa cheti cha kitaaluma ili aweze kutambulika kama Mhasibu na kuweza kufanya kazi nje na ndani ya nchi.

Mkuu wa shule ya Sekondari ya Chumbageni Maua Juma Mkangama akiwatambulisha na kuwakaribisha wafanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) waliofika shuleni hapo kwa ajili ya kuwahamasisha wanafunzi hao kujiunga na masomo ya Uhasibu watakapomaliza masomo yao ya Sekondari.
Afisa Masoko na Mawasiliano Mwandamizi wa NBAA, Magreth Kageya akitoa elimu kuhusu kazi zinazofanywa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Chumbageni iliyopo mkoani Tanga.
Mfanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Sawa Ngendabanka akitoa elimu kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Chumbageni pamoja na kuwahamasisha wanafunzi hao kujiunga na masomo ya Uhasibu watakapomaliza masomo ya Sekondari.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Chumbageni wakiuliza maswali kwa wafanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) waliofika kutoa elimu shuleni hapo mkoani Tanga.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Chumbageni wakifuatilia mafunzo yaliyokuwa yanatolewa na wafanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) waliofika kutoa elimu shuleni hapo mkoani Tanga.
Mkuu wa shule ya Sekondari ya Chumbageni Maua Juma Mkangama pamoja na wafanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Chumbageni mara baada ya kutoa elimu shuleni hapo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad