Afisa Masoko na Mawasiliano Mwandamizi wa NBAA, Magreth Kageya akitoa elimu kuhusu kazi zinazofanywa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) kwa wanafunzi wanaosoma masomo ya biashara wa Shule ya Sekondari ya Coastal iliyopo jijini Tanga.
Mfanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Sawa Ngendabanka akitoa elimu kwa wanafunzi wanaosoma masomo ya biashara wa Shule ya Sekondari ya Coastal pamoja na kuwahamasisha wanafunzi hao kujiunga na masomo ya Uhasibu watakapomaliza masomo ya Sekondari.
Baadhi ya wanafunzi wanaosoma masomo ya biashara wa Shule ya Sekondari ya Coastal wakifuatilia mafunzo yaliyokuwa yanatolewa na wafanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) waliofika kutoa elimu shuleni hapo mkoani Tanga.
Wafanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wanaosoma masomo ya biashara katika Shule ya Sekondari ya Coastal mkoani Tanga.
No comments:
Post a Comment