HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, February 22, 2025

PWANI KUZINDUA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA MAMA SAMIA

  


Na Khadija Kalili Michuzi TV
MKUU wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge amesema kuwa Mkoa wa Pwani utazindua Huduma ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia 'Samia Legal Aid' tarehe 24 Februari 2025 katika Viwanja vya Stendi ya zamani Mailimoja Kibaha.

RC Kunenge amesema hayo leo tarehe 22 Februari 2025 kwenye mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika ofisini kwake Mkoani hapa. Pia ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Pwani kujitokeza kwa wingi kesho Jumatatu kuanzia saa tatu asubuhi.

"Wananchi wote wenye malalamiko wajitokeze kupeleka malalamiko yao yanayohitaji msaada kisheria na nina imani watapata msaada" amesema Kunenge.

Amesema kuwa kwa malalamiko yote yanayohusiana na masuala na ndoa , mirathi, ardhi wote watasikilizwa

Huduma hii inatolewa na Wizara ya Katiba na Sheria.

Tayari Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia imefanyika kwenye Mikoa 19 na Pwani unakua Mkoa wa 20.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad