Na Mwandishi Wetu
MWANAMUZIKI
maarufu katika Muziki wa Injili nchini Rehema Simfukwe amevunja ukimya
kwa mara ya kwanza kwa kuamua kutoa sababu za kutunga wimbo wa Chanzo
ambao umekuwa ukipendwa na kuvuta hisia za watu wengi kutokana na
mashairi yaliyoandikwa katika wimbo huo.
Rehema
Simfukwe tangu alipotoa wimbo huo miaka minne iliyopita hakuwahi kutoa
sababu za kutunga na kuimba wimbo huo lakini ameona sasa ni wakati
muafuaka kuwaambia Watanzania kuhusu wimbo Chanzo.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam Januari 12,2024 wakati wa hafla ya kuelezea sababu
za kuimba wimbo wa Chanzo sambamba na kusherehekea kumbukizi ya
kuzaliwa kwa mtoto wake wa kwanza Dorcas ambaye ametimiza miaka sita
tangu kuzaliwa kwake.
Amemetumia
nafasi hiyo kueleza kuwa Dorcas ndio sababu iliyomfanya yeye kuimba
wimbo wa Chanzo kwani ni mtoto ambaye alimzaa na amekuwa na changamoto
ya kupooza kwa ubongo au mtindio wa ubongo.
“Mungu
amenijaalia watoto watatu lakini duniani huku watu wengi wanajua nina
watoto wawili. Mtoto wangu wa kwanza anaitwa Dorcas ambaye alizaliwa na
changamoto ya kupooza ubongo au mtindio wa ubongo kwa hiyo alikuwa na
changamoto sana katika maisha yake.
“Changamoto
hiyo kwa Dorcas ilisababisha tangu alipozaliwa tukawa na maisha ya
hosipitali siku hadi siku. Nimekuwa nikiimba nyimbo za injili, nafanya
mahojiano na vyombo vya habari kuhusu wimbo wa Chanzo lakini sijawahi
kueleza upande wa pili kuhusu wimbo huu,” amesema mwanamuziki Rehema
Simfukwe.
Amesema
amekuwa kimya muda wote kwasababu alikuwa anasubiri apate kibali kutoka
kwa Mungu kuzungumzia wimbo huo na hiyo ndio sababu ya kutunga na
kuimba wimbo huo ambao unazungumzia maisha halisi ya Mtoto Dorcas.
“Ukiusikiliza
wimbo huu utaona ndani yake kuna ujumbe uliobeba maumivu ya Dorcas na
ndio sababu ya kuimba wimbo huo, nafahamu tangu ulipotoka watu
wameuopokea, na wamekuwa wakiuimba na kuufurahia na nimekuwa nikiulizwa
sababu za kuimba wimbo huu.
“
Nilimuahidi Mungu kuwa sitasema hili mpaka pale atakaponiruhusu na
nimekaa na hii siri kwa miaka kadhaa na ninaamini Mungu amenipa mtoto
Dorcas ili niwe mfano kwa wengine, ili nisaidie wengine wenye watoto
wenye changamoto kama za Dorcas.
Hata
hivyo amesema wakati wakisherehekea kumbukizi ya kuzaliwa kwa mtoto
Dorcas pia ameamua kutangaza kufungua kituo cha kuelea watoto ambao
wanachangamoto ya mtindio wa ubongo. Kituo hicho kitafahamika kwa jina
la Dorcas Home Care Initiative kilichopo Madale jijini Dar es Salaam.
“Wakati
leo tunafurahia miaka sita ya Dorcas naomba nitangaze uwepo wa Dorcas
Homecare Initiative, lengo la kituo hiki ni kupokea watoto wenye
changamoto ya mtindio wa ubongo, na hakutakuwa na gharama yoyote kwani
nimeamua kutoa huduma ya kulea watoto hao na nimeanza na watoto nane.
“Kwa
wale ambao wataguswa basi wanaweza kutuchangia kupitia akaunti ya NBC
074172000439TZS na 074173000101 wakati namba ya benki ya CRDB ni
015C0005PQW00 TZS na namba ya M-pesa ni 0768571613(Dorcas Home Care.”
No comments:
Post a Comment