HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, January 9, 2025

KITUO CHA GESI ASILIA CHA MAWASILIANO KUANZA KUTOA HUDUMA FEBRUARI 03, 2025





Naibu waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Dotto Biteko leo Januari 09, 2025 akitembelea akitembelea kituo cha kujazia gesi katika  vyombo vya usafiri vinavyotumia gesi.


Na Avila Kakingo.
KITUO kituo cha gesi Asilia kilichopo Mawasiliano katika Barabara ya Samnujoma, Ubungo jijini Dar es Salaam kuanza kutoa huduma Februari 03, 2025 katika magari, Pikipiki, Bajai na Taxi zinazotumia mfumo gesi zitaanza kujaza gesi katika kituo hicho.

Na Shilingi Bilioni 18.9 zilizotumika kufanya kazi ya ujenzi wa kituo cha kujazia gesi asilia cha Mawasiliano Samnujoma, Muhimbili pamoja na Kairuki vyote hivyo ni fedha kutoka shirika la maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

Hayo yamesemwa leo Januari 09, 2025 jijini Dar es Salaam na Naibu waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Dotto Biteko wakati wa ziara ya kutembelea kituo cha gesi asilia cha kujaza gesi ambacho kimejengwa TPDC. Amesema mitambo yote inayohitajika imeshawasili na Ujenzi utakamilika ndani ya wiki moja na maandalizi yamekamilika.

"Mkandarasi ametuhakikishia itakapofika Februari 03, 2025 kwa mara ya kwanza magari yatakuwa yatakuja kujaza gesi hapa." Amesema Dkt. Biteko

Amesema malengo ni kuondoa foleni ambazo zinajitokeza katika vituo vya kujazia gesi katika magari, Pikipiki na Bajaji katika jijini la Dar es Salaam.

Amesema mwitikio wa Watanzania kuhama kwenye matumizi ya mafuta kwenda kwenye nishati safi umekuwa mkubwa ndio maana watu wanaotumia vyombo vya usafirishaji wanatumia gesi asilia.

"Na serikali Rais Samia ameshatoa maelekezo ya kujenga vituo vingi zaidi katika jiji la Dar es Salaam ambako ndio matumizi ni mkubwa wa gesi."

Amesema kutajengwa kituo kingine cha kujazia gesi asilia katika vyombo ya usafiri, lakini wakati huo huo kunavituo vingine saba vinajengwa na sekta binafsi.

Amesema nia ni kuona kwamba vituo hivyo vinaongezeka idadi mpaka kufikia vituo 15, wakati huo huo kuwe na vituo vinavyotembea ambavyo vitakuwa morogoro kimoja na Dodoma vitakuwepo viwili.

"Nataka tuwahamishe wananchi kutoka kwenye matumizi ya nishati siyokuwa safi kwenda kwenye nishati safi ambayo Rais Samia ni Kinara wa Nishati safi Afrika na hasa nishati ya kupikia."

Amesema kuwa watahakikisha kuwa vituo hivyo vinajengwa kwa haraka, pia amewapongeza TPDC kwa kazi nzuri wanayoifanya na kuajiri vijana wakitanzania kwaajili ya kusaidia kazi za ujenzi wa kituo hicho.

Akizungumzia matumaini ya ujenzi wa kituo cha gesi asilia kwaajili ya kujaza kwenye vyombo vya usafiri, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba amesema matumaini ni makubwa kwani februari 03,2025 magari yataanza kujaza gesi katika kituo hicho.

Amesema kituo hicho ni kituo mojawapo kilichopo katika mipango ya maendeleo kabla ya kuisha mwaka wa fedha wanatagemea kuwe na vituo vingine saba ambavyo vitakuwa Mbezi Beach, Tegeta, Mwenge, Simu 2000, Muhimbili, Kairuki na kibaha ikiwa na nia ya kuwawezesha wananchi wanaotaka kubadilisha magari yao kutumia gesi au wameshabadilisha waweze kuwa na nishati safi ya gesi katika magari yao.

Amesema mipango ya wizara kwenye eneo la gesi asilia linakwenda vizuri hasa kwenye matumizi ya kawaida.

Licha ya hayo, Mhandisi Mramba amesema wamekubaliana na Wakala wa Mabasi yaendayo haraka (DART) kwamba magari yatayokuja yatakuwa na uwezo wa kutumia gesi asilia.

Kwa upande wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM), Profesa William Anangisye amesema kuwa ujenzi wa kituo cha SNG katika eneo la UDSM utawanufanisha hasa katika kutoa elimu kwa vitendo kwa wanafunzi wa chuo hicho pamoja na fursa mbalimbali zitakazojitokeza kwa wanafunzi wanaosomea masuala ya gesi.

Pia amesema kuwa watahakikisha kituo hicho kipo salama muda wote kutokana na kuwa katika eneo hilo. Na ajira nyingi zitakazopatikana zitasaidia vijana wa kitanzania kwa maendeleo ya taifa kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad