SHULE Sekondari Feza Boys imejivunia uwekezaji iliyofanya katika kumuandaa mwanafunzi kuwa bora baada ya kufaulisha wanafunzi wote kwa kupata daraja la kwanza katika mtihani wa Taifa wa kidato cha nne ulifanyika mwaka 2024, huku zaidi ya asilimia 65 wakipata division 1.7.
Hayo
ameyasema Makamu Mkuu wa Shule ya FEZA Boys, Shabani Mbonde wakati
akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 23,2025 katika shule
hiyo iliyopo Kunduchi Dar es Salaam mara baada ya Baraza la Mitihani
kutangaza matokeo ya kidato cha nne.
Mbone ameleeza kuwa matokeo
hayo hajatokea tu kirahisi bali ni uwekezaji na mazingira ya shule
yanayomtengeza mwanafunzi kuwa bora na walimu wa kutosha ambapo kila
mwalimu ana wastani ya kufundisha wanafunzi 10.
" FEZA SHOOLS
haitoi mwanafunzi bora katika A tu, bali katika nyanja zote.Sisi katika
elimu hatumjengi mwanafunzi kupata A tu lakini pia katika kukabiliana
na hali zote katika maisha kulingana na wakati uliopo.
"Hii yote
inatokana na jitihada mbalimbali za wanafunzi wenyewe na walimu.
Mwanafunzi wetu anakuwa ni kama ametoka kwenye mashine au kiwanda
kilichomjenga katika kupambana na changamoto mbalimbali katika mtihani
na maisha.Tunajivunia wanafunzi wetu na walimu wetu," amesema Makamu
Mkuu huyo.
Aidha Mbonde amesema kama sekta binafsi wanashukuru
serikali kwa kusisitiza suala la elimu na wanaiunga mkono Serikali
katika kuhakikisha elimu inakuwa bora.
Naye Mkuu wa taaluma
msaidizi wa kidato cha tatu na nne, Abdallah Juma ameeleza mbinu
wanazotumia kuwafundisha wanafunzi hao kuwa ni progamu mbalimbali
walizonazo shuleni hapo.
" Sio kwamba sisi vijana wote
tunaowachukua ni wale 'cream' tu bali wanakuja hata wenye uwezo mdogo
tunawatengeneza na wanakiwa sawa na wenzao na wanafaulu kwa pamoja.
"
Matokeo haya yamepatikana kwa njia tofauti, pande zote tatu zina
mchango yaani wazazi, walimu na wanafunzi, pia tuna programu mbalimbali
za masomo kuanzia asubuhi, jioni na hata usiku, pia wanapata muda wa
kucheza", amesema.
Kwa upande mmoja wa wanafunzi wa FEZA BOYS
waliofanya vizuri kwa kupata division one 1.7, Moses Francis, amesema
anamshukuru Mungu kwani mafanikio hayo hayakuja kirahisi ya kupata A
masomo yote 10 ila mazingira ya shule yamechangia ikiwamo kusoma kwa
bidii kama mwanafunzi.
Amefafanua kuwa kutokana na ratiba za
shule zilivyopangiliwa wanapata muda wa kutosha wa kupumzika lakini kuna
kipindi kigumu unatakiwa kusoma sana ili kufaulu mtihani.
"Hii
haipatikani kirahisi, mtu kufaulu lazima kuwe na motisha kuanzia kwa
mwanafunzi wenyewe na mzingira mazuri ya kujifunzia pamoja na
kumtanguliza Mungu.Kila wiki tunafanya mazoezi ya masomo kwa kufanya
test," amesema Moses.
Katika matokeo ya kidato cha nne
yaliyotangazwa leo na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), ufaulu
umeongezeka ambapo jumla ya watahiniwa wa shule 477,262 kati ya 516,695
wenye matokeo sawa na asilimia 92.32 wamefaulu kwa kupata madaraja ya
I,II,III,IV.
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Feza Boys wakishangilia kwa kumbeba mwanafunzi mwenzao,Allan Masaka aliyefanya viziuri katika matokeo ya kidato cha nne kwa kupata ufaulu wa alama A.7 jumla ya wanafuzi woote katika shule hiyo wamepata ufaulu wa alama A .Na,mpiga picha maalumu
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Feza Boys wakishangilia kwa kumbeba mwanafunzi mwenzao,Moses Mwaijande aliyefanya viziuri katika matokeo ya kidato cha nne kwa kupata ufaulu wa alama A.7 jumla ya wanafuzi woote katika shule hiyo wamepata ufaulu wa alama A .Na,mpiga picha maalumu
No comments:
Post a Comment