HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, December 16, 2024

Waziri Jerry Silaa Aagiza Bodi ya TTCL Ilete Mabadiliko, Shirika Lijiendeshe Kibiashara

WAZIRI wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Jerry Silaa ameiagiza Bodi ya Shirika La Mawasiliano Tanzania (TTCL)  kuhakikisha linasimamia vyema shirika  hilo na kuhakikisha liendeshwa kibiashara.

Maagizo hayo ameyatoa leo Desemba 16, 2024 Jijini Dar es Salaam, wakati akizindua Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).

Mhe. Silaa amemtaka Mwenyekiti wa Bodi hiyo David  Nchimbi  kutengeneza mpango utakalitoa Shirika lilipo na kulipeleka kwenye  uendeshaji kibiashara ikiwa ni kutekeleza maagizonya Rais Samia,

"Rais Samia Suluhu Hassan alielekeza shirika kuhakikisha linaendeshwa kibiashara hivyo  Mwenyekiti atengeneze mpango utakaotutoa tulipo na kupeleka shirika kwenye uendeshaji kibiashara " amesema Mhe. Silaa.

Aidha Mhe. Silaa amesema serikali  imewekeza  fedha nyingi kwenye miundombinu ya  mawasiliano   ya Taifa   ikiwemo mkongo wa taifa ambao umeunganisha karibu nchi nzima  na kuna miradi mbalimbali na kuna kuna miradi mikubwa ya mawasiliano mradi wa  ktuo cha Taifa cha data hivyo ni nia ya Rais Samia  kuona uwekezaji huo mkubwa uliofanywa kwa fedha za wananchi  uweze  kuleta tija kwa kujiendesha kibiashara na kuiona ile thamani ya fedha iliyotolewa.

Amesema iwapo Shirika likiendeshwa vyema linaweza kukuza sekta mbalimbali  na kuleta mapinduzi makubwa ikwenye uchumi wa nchi.

"Hivyo  Mwenyekiti na wajumbe  tekelezani hayo na  ninawaahidi  milango ya wizara iko wazi, na mtambue  uendeshaji wa shirika uko chini ya bodi hivyo uwajibikaji uko chini ya mabega yenu siimamieni menejimenti vizuri   ili tufike tuendako" amesema,

Kwa upande wake Mwenyekiti wa  bodi hiyo Nchimbi ameshukuru Rais Samia Suluhu Hassan  kumteua katika nafasi hiyo  na kuahidi kuwa na shirika jipya  na kulipeleka mbele  zaidi na kwa kasi.

Amesema wajumbe wana uwezo mkubwa na wamesikia maelekezo  yaliyotolewa na watayafanyia kazi na hakuna litakalowashinda .









No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad