HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 12, 2024

PROF. JANABI ASISITIZA JAMII KUJIKINGA NA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA

 

Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili ambaye pia ni Mshauri wa Rais kwenye masuala ya Afya na Tiba, Prof. Mohamed Janabi amesema ni muhimu jamii ikajikita katika kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza kwakuwa magonjwa hayo yana usumbufu na gharama kubwa kuyatibu.


Prof. Janabi ametoa wito huo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa salamu zake za Krismas kwa jamii na kuongeza kuwa yeye binafsi amejikita katika kutoa elimu kwa jamii kwa kutambua madhara ya magonjwa yasiyoambukiza kwa jamii.

Prof. Janabi amebainisha kuwa takribani watu milioni 34.6 hufariki kila mwaka duniani kutokana na magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo saratani, magonjwa ya moyo, shinikizo la damu, kiharusi na magonjwa ya kisukari.

Prof. Janabi ameongeza kuwa magonjwa ya moyo, shinikizo la damu, kiharusi na ugonjwa wa kisukari huua asilimia 364 zaidi ya ugonjwa wa saratani kwa mwaka, hivyo jamii inatakiwa kuweka msukumo wa kukabiliana magonjwa haya kutokana na madhara yake.

“Suluhisho la magonjwa haya ni kubadili mtindo wetu wa maisha kwa kulala sawasawa, kufanya mazoezi, kuongeza mbogamboga, matunda na kupunguza msongo wa mawazo. Na kwa kiasi kikubwa magonjwa haya yanaathiri nchi hizi zinazoendelea” ameongea Prof. Janabi

Prof. Janabi amesisitiza kuwa hajakataza watu kula lakini anachoshauri watu kula kwa kiasi, kula chakula bora na kula chakula pale mtu anapohisi kwa afya, hivyo ni jukumu la mtu kutengeneza utaratibu mzuri wa kula.


 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad