Na MWANDISHI WETU.
Mfuko
wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umetoa semina kwa waajiri wa sekta
binafsi wanaohudumiwa na Ofisi ya NSSF Mkoa wa Ubungo, Dar es Salaam.
Semina
hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika Ofisi za NSSF Ubungo ikiwa na
lengo la kuwakumbusha waajiri majukumu yao yakiwemo kusajili
wafanyakazi wao na kuwasilisha michango kwa wakati kwani hilo ni takwa
la kisheria.
Katika semina hiyo mada mbalimbali zilitolewa ikiwa
ni pamoja na matakwa ya Sheria ya Mfuko na Matumizi ya Mifumo ya Tehama
iliyoboreshwa (Employer Portal). Vilevile, mada kutoka Ofisi ya TAKUKURU
Wilaya ya Ubungo ziliwasilishwa na Bi. Devotha Mihayo, ambaye ni Mkuu
Ofisi ya TAKUKURU Wilaya ya Ubungo.
Akifungua semina hiyo, Meneja
wa NSSF Mkoa wa Ubungo, CPA. Joseph Fungo amewashukuru waajiri wa sekta
binafsi kwa kushiriki semina hiyo yenye lengo la kutoa elimu ya hifadhi
ya jamii kwa waajiri pamoja na kuwakumbusha waajiri kutimiza wajibu wao
kwa mujibu wa sheria ikiwa ni pamoja kutoa taarifa za wafanyakazi
wasiosajiliwa ili Mfuko uweze kuwasajili na kisha kuwasilisha michango
kwa wakati
Aidha, CPA. Fungo alieleza kuwa suala la kutoa elimu
kwa wanachama na waajiri wa sekta binafsi wa mkoa huo litaimarisha
ushirikiano kwa waajiri na Mfuko na kuongeza mafanikio ya utoaji wa
huduma bora kwa wanachama na wadau kwa ujumla.
Kwa upande wake,
Bw. Geofrey Ngwembe, Afisa Sheria wa NSSF ametumia semina hiyo
kuwakumbusha waajiri hao kutekeleza wajibu wao kisheria katika
kuhakikisha michango ya wanachama inawasilishwa kwa wakati pamoja na
kuwajengea uelewa kuhusu maswala mbalimbali yanayohusu sheria ya hifadhi
ya jamii.
No comments:
Post a Comment