MWISHONI mwa wiki katika viwanja vya TFF vilivyopo makao makuu yao KIsarawe II, Kigamboni, Dar Es Salaam viliwakutanisha wachezaji nguli maveterani wa soka wa Bara na Visiwani.
Wachezaji hao walikutana kwenye bonanza la awamu ya kwanza lililoandaliwa na Kibada Veterans ambapo Rais wa TFF, Wallace Karia alikuwa mgeni rasmi.
Mbali ya Karia viongozi wengine walikuwa Mwenyekiti wa Kibada Veterans ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa DRFA, Benny Kisaka, Mwenyekiti wa chama cha soka Ilala ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya DRFA, Mussa Kondo na Mwenyekiti wa chama cha soka Ubungo, Hashim Sozigwa, na kamati nzima ya utendaji ya Kibada Veterans.
Wachezaji veterans nguli waliotoka Zanzibar ni pamoja na winga wa muda mrefu wa Zanzibar Hereos... na Taifa Star, Nassoro Mwinyi Bwanga ambae pia alipata kuzichezea Black Fighter, Ujamaa na ligi ya kulipwa nchini Oman.
Wengine ni Sabri Ramadhan China (Mlandege, Zbar Herous na Taifa Stars), Abdi Kassim Babi (Mtibwa, Yanga, Zbar Herous na Taifa Stars), Ramadhan Hamza Kidilu (Sigara, Mtibwa, Mlandege na Zanzibar herous) na Mahmoud Hamza aliyepata kuzichezea Mlandege na Z'bar Hereous.
Sanjari pia na Shem Frank aliyepata kukipiga Mlandege na Zanzibar Hereous, Duwa Said (Small Simba, Simba na Taifa Stars), Abdulkadir Tash alipata kucheza Miembeni, Small Simba, Malindi, Yanga, Z'bar hereous na Taifa Stars.
Galactico's wao waliongozwa na George Magere Masatu aliyechezea Coop na Pamba za Mwanza, Simba na Taifa Star, ikimbukwe pia ndiye libero aliyecheza fainali ya CAF ambapo Simba ilipoteza kwa Stella Abdjan.
Wengine sanjari na Albert Sengo, Abdallah Kaburu (Ushirika, Pilsner, Ndovu na Yanga), na Jumanne Njovu (Ashanti Untd), Mtwa Kihwelo, Simion Alando. Haruna Moshi Boban,
Wenyeji Kibada waliongozwa na Malota Soma na Isihaka Hassan Chuku kwenye benchi la ufundi.
Baadhi ya nguli Waliochezea ni pamoja na Juma Kaseja, Amani Simba, Swed Mkwabi, Gadau, Juma Pinto, Said Chopa, Gwandumi, Raymond, Arnatoly, Silumbe na nahodha Greyson Sakaya.
Mchezaji bora wa bonanza hilo aliibuka Abdulkadir Tash, mfungaji bora walifungana kwa mabao 6 kila mmoja, Chopa wa Kibada na Philipo wa Zanzibar ambapo kipa Amani Simba wa Kibada Veterans aliibuka kipa bora kwa kuwa na cleen sheet nyingi.
No comments:
Post a Comment