Na Mwandishi wetu
Mashabiki wa soka wa Tanzania, sasa wanaweza kujishindia
zawadi mbalimbali ikiwa pamoja na fedha kupitia kampeni ya Amsha Amsha
iliyozinduliwa na kampuni ya michezo ya kubashiri ya M-Bet Tanzania na
Halotel.
Meneja Masoko wa M-Bet, Levis Paul aliema kuwa mbali ya
zawadi ya fedha ya Sh50,000 kwa washindi wawili kwa siku, pia mashabiki
wa soka wanaweza kujishindia fedha taslimu, simu janja, na televisheni
za kisasa.
Paul alisema kuwa kampeni hiyo imelenga kuwazawadia
wateja wao ambapo pia wanaweza kushindia fedha kwa kubashiri matokeo ya
mechi katika ligi mbalimbali duniani.
“Washindi wawili wa kila
siku watajishindia Sh50,000, ambapo jumla ya Sh6,000,000 zimetengwa kwa
kipindi hiki cha sikukuu,” alisema Paul.
Aliongeza kuwa kila
mwisho wa wiki kutakuwa na droo maalum ambapo washindi wawili
watajishindia simu janja ya Samsung A-Series yenye thamani ya Sh500,000.
Zaidi
ya hayo, wateja pia watapata nafasi ya kujishindia televisheni za
kisasa aina ya Hisense zenye thamani ya Sh1.2 milioni kila moja, ambapo
jumla ya televisheni nane zitatolewa katika kipindi cha miezi mitatu ya
promosheni.
Alisema kuwa shabiki wa soka anaweza kuingia kwenye
droo kwa kujisajili kupitia tovuti yao, www.m-bet.co.tz, kuweka pesa
kupitia HaloPesa, na kubeti kwa dau la kuanzia Sh2,000 ili kuingia
kwenye droo.
Kwa upande wake, Afisa Masoko wa HaloPesa, Aidat
Lwiza, alisema, “Tunafurahi kushirikiana na M-Bet kwenye promosheni hii.
Lengo letu ni kutoa fursa kwa wateja kufurahia michezo ya kubashiri
kupitia HaloPesa, ambayo ni njia rahisi na salama ya kufanya malipo.
Promosheni hii itaunganisha burudani ya kubashiri na urahisi wa huduma
za malipo ya simu.”
Lwiza aliongeza kuwa promosheni hii
itawawezesha wateja wa HaloPesa kufurahia huduma za M-Bet na kuingia
kwenye droo za zawadi za kila siku, wiki, na mwezi.
3. Meneja Masoko wa Kampuni ya michezo ya kubashiri ya M-BET Tanzania, Levis Paul (kushoto) na Afisa Masoko wa HaloPesa Aidat Lwiza wakionyesha kifurushi kilichojaa zawadi ambazo watazawadiwa wateja wao kupitia kampeni ya Amsha Amsha
Meneja Masoko wa Kampuni ya michezo ya kubashiri ya M-BET Tanzania, Levis Paul (kulia) akizungumzia kampeni ya Amsha Amsha ambayo wanashirikiana na kampuni ya simu ya teja na Halotel kupitia HaloPesa. Kushoto ni Afisa Masoko wa HaloPesa, Aidat Lwiza.
4. Wafanyakazi wa kampuni ya michezo ya kubashiri ya M-BET Tanzania na Halotel Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja huku wakionyesha picha za zawadi mbalimbali katika kampeni ya Amsha Amsha.
No comments:
Post a Comment