Jengo la Kibaha Shopping Mall linavyoonekana kwa mbele.
Na Khadija Kalili, Michuzi TV
MKUU wa Wilaya ya Kibaha Nickson Simon atakua mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa soko la kisasa litakalofahamika kwa jina la 'Kibaha Shopping Mall'.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mchana wa leo tarehe 6,Desemba ,2024 Afisa Biashara Halmashauri ya Mji Kibaha Sabrina Kikoti amesema kuwa kwa niaba ya Mkurugenzi wao wanatoa shukran kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa aluoufanya wa soko hili.
"Ujenzi wa soko hili umegharimu kiasi cha Bil.8 fedha ambazo zimetoka serikali kuu" amesema Sabrina.
Aidha ameongeza kwa kusema kuwa ndani ya soko hilo wafanyabiashara mbalimbali wamepata fursa za kupangishwa na vyumba vyote vimejaa.
Tutakuwa na wafanyabiashara wenye nembo zote kubwa hapo baadaye pamoja na huduma za kibenki nazo zitapatikana.
Mhasibu wa Halmashauri ya Mji Kibaha Luna Kakuru amesema huduma zingine zitakazopatikani pamoja na michezo ya watoto, kutakuwa na huduma watoa vyakula na vinywaji mbalimbali (bar).
"Huu ni mradi wa kimkakati pia matarajio yetu ni kukusanya kiasi cha Mil.660 kwa mwaka" anesema Kakuru.
Mfanyabiashara Charles Chandika ambaye anaduka la bidhaa za kilimo na mifugo amewahakikishia wakaazi wa kibaha kupata huduma bora.
Wakati huohuo Lydia Vicent ambaye anamiliki duka la vitenge na nguo amesema anamshkuru rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwekeza Mji wa Kibaha jambo ambalo yeyeamekuwa miongoni mwa wakaazi waliopata fursa ya kufanya biashara kwenye eneo la kisasa Kibaha Shopping Mall.
Wasanii mbalimbali watapamva uzinduzi huu ambao ni kundi la Weusi, Maarifa,Smata.
Mhasibu wa Halmashauri ya Mji Kibaha Luna Kakuru.
Afisa Biashara Halmashauri ya Mji Kibaha Sabrina Kikoti.
kibaha sehemu gani
ReplyDelete