Dhumuni la Ziara hiyo ni kuona changamoto zilizopo na kuzitafutia mkakati na kuielekeza Menejimenti ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao na kuwezesha biashara.
Aidha Bodi hiyo imefanya ziara hiyo Desemba 10 katika mpaka wa Tunduma mkoani Songwe na Desemba 11 kwenye mpaka wa Kasumulu mkoani Mbeya.
Pamoja na hayo Bodi imeielekeza menejimenti ya TBS kuja na mikakati ya bidhaa zinazoingia kupitia njia za panya na kukwepa ukaguzi ikiwa ni pamoja na kuendelea kutoa elimu ya madhara ya kutumia bidhaa ambazo hazijathibitishwa ubora wake na TBS.














No comments:
Post a Comment