Mkuu
wa Mawasiliano na Uhusiano kutoka Airtel, Jackson Mmbando na Meneja
Huduma kwa Wateja kutoka Airtel, Celine Njuju wakionesha moja ya zawadi
ambazo zitatolewa katika msimu huu wa sikukuu.
Mkuu
wa Mawasiliano na Uhusiano kutoka Airtel, Jackson Mmbando akizungumza
jijini Dar Es Salaam leo Desemba 17, 2024, ikiwa ni katika kusheherekea
sikukuu ya Christimas ambapo watatoa zawadi mbalimbali kwa wateja wao.
Meneja
Huduma kwa Wateja kutoka Airtel, Celine Njuju akizungumza jijini Dar Es
Salaam leo Desemba 17, 2024, ikiwa ni katika kusheherekea sikukuu ya
Christimas ambapo watatoa zawadi mbalimbali kwa wateja wao.
KAMPUNI ya Airtel Tanzania imezindua promosheni ya Airtel Santa Mizawadi nchini Kwa kuwazawadia wateja na mawakala.
Akizungumza
jijini Dar Es Salaam leo Desemba 17, 2024, ikiwa ni katika
kusheherekea sikukuu ya Christimas, Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano,
Jackson Mmbando amesema Airtel Tanzania inaanza msimu huu wa sikukuu na
Airtel Santa Mizawadi ambayo ni promosheni maalum yakutoa shukrani na
kuwazadia wateja na mawakala wote wanaoendelea kutumia huduma za Airtel
katika msimu wa sikukuu.
Airtel
Santa Mizawadi ni ipo kabambe na itawapatia washindi fursa ya kuondoka
na zawadi kemkem ikiwemo pocket WiFi, simu janja, pikipiki, runinga na
pesa Taslim hadi shilingi milioni moja.
"Jinsi
ya kushirikina kujishindia Mizawadi ya Airtel Santa Mizawadi, ikiwa
awewe ni Wakala wa Airtel unatakiwa tu kufanya miamala ya kuweka na
kutoa fedha, ambapo pia ili Mteja aweze kuingia kwenye droo anatakiwa tu
kufanya miamala kama vile kununua bando, Kutuma pesa, kutoa pesa,
kulipa bili, kufanya miamala ya kibenki, kutuma au kupokea pesa nje ya
nchi, kununua muda wa maongezi au vifurushi kupitia *149*99#, *150*60#,
au kwa kutumia ‘My Airtel App’."
Mmbando,
ameeleza kuwa Promosheni ya Airtel Santa Mizawadi ni inalenga
kuwashukuru wateja na mawakala waaminifu na wanaoendelea kutumia Airtel
katika msimu wote huu wa sikukuu.
“Kupitia
Promosheni ya Airtel Santa Mizawadi tunasambaza upendo na kunogesha
sikukuu kwa wateja na mawakala wetu wetu ambao wamekuwa na mchango
mkubwa katika mafanikio yetu,” amesema Mmbando.
Amesisitiza
kuwa Airtel inaendelea kujidhatiti kutoa huduma za kipekee katika msimu
wa sikukuu huku akidokeza kuwa kila muamala unaofanyika unatoa nafasi
kwa wateja au mawakala kujishindia zawadi zitakazoboresha Maisha.
Kwa
upande wake Meneja Huduma kwa Wateja, Celine Njuju amesema ... “Airtel
tunawadhamini sana wateja wetu, Tusingefika hapa tulipo leo bila ya
wateja na mawakala wetu, Airtel Santa Mizawadi ni promosheni kabambe
kwa kuwa itanogesha balozi wetu, mtamuona Mr SANTA wetu akitembelea
baadhi ya mitaa yetu kuhakikisha wateja na mawakala wanapata pia zawadi
za papo kwa hapo, ikiwa utabahatika kukutana nae basi nakuahidi
atanogesha msimu wako wa sikukuu vizuri ufurahie wewe na wapendwa
wako.”
Amesisitiza
kuwa washindi wa Airtel Santa Mizawadi watapatikana kupitia Droo za
zitakazochezwa kila wiki mara moja ambapo washindi wote watapigiwa simu
kupitia namba maalum ya Airtel 100.
No comments:
Post a Comment