Vituo vya taarifa na Maarifa kutoka mikoa Zaidi ya 10 na Halmashauri mbalimbali wamekutanishwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), na kujadiliana juu ya hali ya ushiriki wa wanawake kwenye nafasi za uongozi hasa uchaguzi wa serikali za Mitaa na kutoa mapendekezo ambayo yataweza kubadilisha baadhi ya sera, sheria na mifumo ya uchagujzi.
Miongoni mwa mapendekezo hayo ni Kanuni na taratibu za uchaguzi wa ndani ya vyama vya siasa zirekebishwe ili chaguzi ziweke kuwa na haki na usawa
Kuwepo na utaratibu wa wazi na kikanuni wa utoaji wa elimu ua uchaguzi, utekelezaji wa kanuni, sheria na miongozo itakayozuia vitendo vya rushwa ya pesa, ngono pamoja na udhalilishaji wa kijinsia ikiwepo watu kujua haki na wajibu wao wakati wa uchaguzi ndani ya vyama.
Kupambana na kutokomeza mifumo kandamizi ili kukuza usawa wa kijinsia na ushiriki wa wanawake katika uongozi
Serikali na ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa usimamie vyama ili viondoe baadhi ya gharama na michango inayoelekezwa kwa wagombea nafasi za uongozi ambayo inakwamisha wanawake kujitokeza kugombea
Kuwepo mfumo ndani ya vyama wa kuwawezesha wanawake wanaogombea hasa rasilimali fedha ili kumudu gharama
Vituo vya taarifa na Maarifa ziweke mpango na utaratubu wa kuwapigania na kuwasaidia wanawake wanaogombea ili washinde bila kujali itikadi za vyama vyao
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) wakiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki kutoka Vituo vya Taarifa na Maarifa mara baada ya kumaliza mafunzo ya siku tatu yaliyofanyika katika ofisi zake zilizopo Mabibo jijini Dar es Salaam.
Mwezeshaji wa Mafunzo Deo Temba akizungumza namna Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) ulivyojikita na kuendelea kutoa elimu kwa jamii kwa kutumia vituo vya Taarifa na Maarifa ili kuleta usawa wa kijinsia hasa ushirikishwaji wa wanawake kwenye ngazi za uongozi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Baadhi ya washiriki kutoka Vituo vya Taarifa na Maarifa pamoja wakifuatilia mada kutoka kwa wataalam wa TGNP kwenye mafunzo ya siku tatu yanayofanyika katika ofisi zake zilizopo Mabibo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment