HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 21, 2024

TCAA YASHIRIKI NA KUTOA MADA KATIKA MKUTANO WA JUMUIYA YA WATAFITI WA AFRIKA MASHARIKI


Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imeshiriki na kutoa mada katika mkutano wa 16 wa Jumuiya ya Watafiti wa Afrika Mashariki (ORSEA) iliyofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM).
Mada hiyo ya TCAA ilielezea mchango wa kiuendeshaji wa Mamlaka pamoja na majukumu yake ya kiutendaji pamoja na wa kiudhibiti imetolewa jijini Dar es saalam Novemba 21,2024 na Mchambuzi Biashara Mkuu Bw. Henry Machoke.

Katika mada hiyo Bw. Machoke aliainisha namna mashirika ya ndege nchini yanavyopanda na kushuka kibiashara na kugusia juu ya mikakati mbalimbali ya TCAA kwa niaba ya Tanzania inavyohakikisha Usafiri wa Anga nchini unaendelea kuimarika ikiwemo kupata alama za juu katika viwango vya kimataifa vya Shirika la Usafiri wa Anga Duniani(ICAO) katika maeneo ya ulinzi na usalama.

Bw. Machoke pia alitoa wito kwa jumuiya hiyo ya ORSEA kuangalia namna itakavyochangia kama mshirika wa TCAA katika kuja na mikakati mbalimbali ya kuondoa, kupunguza ama kuondoa kabisa changamoto hizo.

Utoaji wa mada hiyo ni sehemu ya mikakati mahususi ya TCAA ya kujitangaza na kuwa karibu na wadau wake kutoka sekta mbalimbali.

Mkutano huo umehudhuriwa na wahadhiri mbalimbali pamoja na wanafunzi kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam na vyuo vingine vya Afrika Mashariki.
Mchambuzi Biashara Mkuu  kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw. Henry Machoke akiwasilisha mada kuhusu uendeshaji wa Mamlaka hiyo, majukumu yake ya kiutendaji pamoja na wa kiudhibiti katika mkutano wa 16 wa Jumuiya ya Watafiti wa Afrika Mashariki (ORSEA) uliofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM).
Baadhi ya washiriki kutoka taasisi mbalimbali wakifuatilia mada katika mkutano wa 16 wa Jumuiya ya Watafiti wa Afrika Mashariki (ORSEA) uliofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM).
Picha ya pamoja


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad