HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 26, 2024

TANAPA KIDEDEA MASHINDANO YA RIADHA - SHIMMUTA 2024

Na:Zaynab Ally - TANGA

Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limeibuka mshindi wa kwanza wa jumla katika mchezo wa riadha kwa wanaume kwenye mashindano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi, na Makampuni Binafsi (SHIMMUTA) 2024.

Katika hafla ya kutangaza washindi mbalimbali kutoka taasisi zilizoshiriki, Katibu Mkuu wa SHIMMUTA Dkt Maswet Masinda alimtangaza Bw. Elibariki Buko kutoka TANAPA kama mshindi wa mchezo wa riadha, akiwashinda washiriki kutoka taasisi zaidi ya 90 zilizoshiriki.

Elibariki Buko aliibuka mshindi katika vipengele vya mita 5000, mita 1500, na mita 800 na kuitangaza vyema TANAPA katika Mchezo wa riadha.

Mashindano ya SHIMMUTA 2024, yaliyosajiliwa na Baraza la Michezo Tanzania (BMT), yamekuwa ya kihistoria kwa TANAPA, ambayo ilitwaa medali zote katika mbio za wanaume, huku TANAPA ikizawadiwa tena medali mbili katika mbio za wanawake.

Mashindano hayo yalifunguliwa rasmi Novemba 10, 2024 na Dkt Dotto Biteko naibu waziri mkuu, yamefungwa jana Novemba 24, 2024, na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Stanslaus Nyongo, aidha katika mashindano hayo yaliyofanyika Jijini Tanga jumla ya watumishi 4,720 kutoka mashirika ya umma 96 walishiriki.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad