HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 18, 2024

Serikali Yatoa Mwongozo wa Utoaji Misaada kwa Wahanga wa Kariakoo kupitia Akaunti Maalumu

NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

UTARATIBU wa utoaji wa msaada wa kifedha kwaajili ya kusaidia walioathirika na kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo Jijini Dar es Salaam zitaelekezwa kwenye akaunti maalumu ya maafa 9921159801ambayo ipo BoT na inashughulikiwa na ofisi ya Waziri Mkuu .

Hayo yameelezwa leo Novemba 18, 2024 Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jim Yonazi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu haki inayoendelea katika zoezi la uokoaji.

Amesema akaunti hiyo ni pekee nchini ambayo inakusanya misaada ya kifedha kwaajhili ya maafa.

"Kuna watu wana nia njema kabisa kwaajili ya kuwasaidia Watanzania, lakini naomba tujizuie kabisa kukusanya michango ya kifedha kutoka kwa mtu yeyote bila kupitia akaunti hii". Amesema Dkt. Yonazi.

Aidha amesema akaunti hiyo ni maalumu imethibitishwa na serikali ili kuweza kuhakikisha misaada inawafikia walengwa na inatimiza malengo ya kutoa misaada hiyo.

Amesema kwasasa operesheni inaendelea mpaka pale watakapokamilisha zoezi la kuokoa baadhi ya watu ambao bado hawajaokolewa.






No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad