HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, November 29, 2024

RAIS RUTO AWASILI NCHINI KUSHIRIKI MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. William Ruto amewasili nchini leo tarehe 29 Novemba 2024 kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 24 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika jijini Arusha tarehe 29 na 30 Novemba 2024.

Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Mhe. Rais Ruto amepokelewa na Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi.

Mkutano huo wa Wakuu wa Nchi umetanguliwa na Kikao cha Ngazi ya Juu kuadhimisha miaka 25 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yenye kaulimbiu isemayo "Miaka 25 ya EAC: Tafakari ya tulikotoka na matarajio ya tunapokwenda"


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad